27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Bodaboda auawa, atobolewa macho

Abdallah Amiri-Igunga

KIJANA mmoja mkazi wa Mtaa wa Stoo Kata ya Igunga mjini wilayani Igunga Mkoa wa Tabora, Maiko Samweli (20) ambaye pia ni dreva bodaboda, ameuawa na watu wasiojulikana na kuchomwa macho kisha pikipiki yake kuporwa.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Igunga, Robert Mwagala alisema tukio hilo lilitokea Machi 23 mwaka huu ambapo kijana huyo mara ya mwisho alipata abiria aliyetaka kupelekwa Kitongoji cha Makomero.

Alisema kijana huyo alipompeleka mteja huyo hakurudi nyumbani hadi Machi 24 saa nne asubuhi ambapo mwili wake ulipookotwa na wachungaji wa ng’ombe ukiwa kwenye porini nje kidogo na Mji wa Igunga.

Mwagala alisema wachungaji hao wa ng’ombe walitoa taarifa polisi ambao waliuchukua hadi hospitali ya Wilaya ya Igunga ambako ulihifadhiwa.

Mwagala alisema ilipofika saa sita mchana siku hiyo, vijana wengine wa bodaboda waliutambua mwili huo.

Baba mdogo wa marehemu, Enock Samweli, alisema mwanaye Maiko Abel alitoweka Machi 23 muda wa jioni.

“Mimi nilipigiwa simu nikiambiwa mtoto wangu amefariki na nilipofika hospitali ya wilaya nilimtambua mwanangu lakini alikuwa ametobolewa macho yote huku kisogo chake kikiwa kimebonyea, kwa kweli inauma sana mtoto wangu ameuawa kikatili,” alisema.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Igunga, Merchades Magongo, alithibitisha kupokea mwili huo ukiwa umetobolewa macho yote.

 “Ni kweli tumepokea mwili wa kijana Machi 24 saa tano asubuhi, Machi 25 ndugu walikabidhiwa kwa ajili ya mazishi ambayo yalifanyika makaburi ya Masanga,” alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles