31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 5, 2024

Contact us: [email protected]

Bod boda 20 mbaroni kwa kushambulia mwendo kasi

LEONARD MANG’OHA NA RAHMA SWAI (TSJ) -DAR ESSALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia waendesha pikipiki maarufu bodaboda 20 kwa tuhuma za kulishambulia basi la mwendo kasilenye namba T 155 DGW kwa mawe na kusababisha uharibifu.

Akizungumzana waandishi wa habari Dar es Salaam jana Kamanda Polisi Kanda Maalumu Dar esSalaam, Lazaro Mambosasa, alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Desemba 8 saa 2:15 usiku katika eneo la Manzese Tiptop.

Mambosasa alisema waendesha pikipiki hao walilishambulia basi hilo baada ya pikipiki yenye namba za usajili MC 964 BYN kuligonga basi hilo na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo waliokuwa wamepakiwa kwa mfumo wa ‘mishikaki’ hukudereva wake akifariki dunia wakati akipelekwa hospitali.

“Pikipiki hiyo ikiwa inapita katika barabara ya mwendokasi iligonga basi lamwendokasi na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo ambao ni abiria wa pikipiki hiyo, dereva wake alijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali nabaadaye alifariki akiwa anaendelea kupatiwa matibabu.

“Baada ya ajali hiyo kutokea madereva bodaboda wanaopaki kandokando ya barabara hiyo walianza kumshambulia kwa mawe dereva wa basi hilona kusababisha uharibifu wa gari hilo.

“Jeshila polisi linatoa onyo kali kwa madereva wote wa vyombo vya moto  kuacha mara moja kutumia barabara za mabasi ya mwendo kasiili kuepusha ajali ambazo zinaepukika,” alisema.

Kutokana na tukio hilo Mambosasa alipiga marufuku vyombo vyote vya moto yakiwamo magariya Serikali kutumia barabara hiyo, huku magari ya kubebea wagonjwa yakiruhusiwa kutumia barabara hiyo pale tu yanapokuwa yanawahisha mgonjwa ili kuokoa maishayake.

Aliongeza kuwa hawatamwonea huruma mtu yeyote atakayekamatwa akitumia barabara hizo na hawatamtoza mtu yeyote faini kwa sababu wako baadhi ya watu wanaandaa faini nakisha kwenda kuvunja sheria.

Wakamatwa na meno ya tembo

Katika tukio jingine polisi inawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na vipande20 vya meno ya tembo.

Kamanda Mambosasa alisema tukio hilo lililokea Desemba 10 mwaka huu saa 3:45 usiku wa maeneo ya Kigogo Fresh Ukonga, baada ya kupata taarifa kuwa kuna watuwanao jihusisha na biashara hiyo ya nyara za serikali hivyo wakaweka mtego nakufanikiwa kuwakamata.

Aliwataja waliokamatwa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na Salehe Iddi (57), Waziri Ibrahimu(40) wote wakazi wa Vingunguti na Bertha Nelson (38) mkazi wa Yombo.

“Watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa kwa kushirikiana na maofisa wa maliasili nautalii na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhumazinazowakabili” alisema Mambosasa.

Wakati huo huo Mambosasa alisema jeshi hilo limekamata silaha mbili aina ya Shortgun Pump Action zenye namba za usajili P-913581 TZ CAR 76456 na P-

625302 TZ CAR 76467 na risasi kumi na saba.

Alisema silaha hizo zilikamatwa Novemba 29 mwaka huu Nov saa 10 :30 alfajiri maeneo ya Kinyerezi Kanga zikiwa zimetelekezwa kwenye mfuko mweusi waplastiki na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao hufanya matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

“Natoa wito kwa watu wote wanaomiliki silaha isivyo halali na kuzitumia katika matukioya kihalifu wazisalimishe haraka sana silaha hizo katika kituo chochotecha polisi kabla hawajakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwanioparesheni ya  kuwasaka wahalifu wanaotumia silaha ni endelevu,” alisemaMambosasa.

Aidha Mambosasa alisema katika kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka jeshi lapolisi limeimarisha ulinzi maeneo yote ya jiji hususani katika taasisi mbalimbali za fedha kama vole benki na maduka ya kubadilishia fedha zakigeni na sehemu zenye mkusanyiko wa 

maduka mengi kama Mlimani City.

“Kama mnavyofahamu katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mwaka kumekuwa nabaadhi ya watu ambao hujitafuta kipato kwa njia isiyo halal kwa kufanya vitendo vya uhalifu,hivyo kutokana na hali hiyo jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha hakuna tukio lolote la uhalifu litakalojitokeza katika kipindi hiki cha maandalizi ya Christmas na mwakampya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles