Bocco, Kagere watwaa tuzo

0
2789

Winfrida Mtoi, Dar es salaam

WASHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere na John Bocco, wamechaguliwa kuwa wachezaji bora wa tuzo ya Marchi na Juni wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kagere amechukua tuzo ya Machi, akiwashinda Paul Nonga wa Lipuli na Never Tigere wa Azam, alioingia nao fainali.

Bocco   amechaguliwa mchezaji bora wa Juni, akiwashinda Atupele Green wa Biashara United na Martin Kiggi wa Alliance FC.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),tuzo ya kocha bora wa mwezi imechukuliwa na Hererimana Haruna wa KMC, aliyechukua ya Marchi na Kess Mziray wa Alliance ametwaa ya June.

Haruna amechukua tuzo hiyo kwa kuwashinda Sven Vandenbroeck wa Simba na Khalid Adam wa Mwadui , huku Mziray akiwashinda  Sven na Luc Eymael wa Yanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here