28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Bocco awatuliza mashabiki Azam

John-Bocco-1-e1438774780905ADAM MKWEPU NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco amewatuliza mashabiki wa timu hiyo na kuwataka wasubiri ushindi wa kishindo watakapocheza na Majimaji keshokutwa katika Uwanja wa Majimaji, Songea.

Azam ilipata matokeo ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba Jumamosi iliyopita na kufikisha pointi 26 zilizoifanya ishuke hadi nafasi ya pili na kuwapa wapinzani wao Yanga nafasi ya kurudi kileleni kwa kujikusanyia pointi 27.

Akizungumza na MTANZANIA jana nyota huyo aliyefunga mabao matano Ligi Kuu, alikiri kuwa mchezo wa keshokutwa utakuwa mgumu lakini akawaondoa hofu mashabiki na kuwataka wasubiri matokeo ya ushindi.

“Mchezo dhidi ya Majimaji utakuwa mgumu kutokana na kila timu kusaka pointi tatu muhimu, lakini tunatarajia kupata matokeo mazuri ugenini ili tuweze kurejea kileleni na kuendelea kuongoza ligi,” alisema.

Straika huyo alieleza kuwa ni vugumu kuzungumzia mwenendo wa ligi kwa sasa na kufanya utabiri kwani kila timu inajitahidi kutafuta mbinu za ushindi kulingana na mipango waliyojiwekea.

“Siwezi kuzisemea timu nyingine na wachezaji wake kwa kuwa mipango inatofautiana na kila mmoja anafanya linalowezekana ili kupata matokeo mazuri,” alisema.

Kwa upande wake, ofisa habari wa klabu hiyo, Jaffar Idd, alisema Azam ina uhakika wa kuondoka na pointi zote tatu dhidi ya Majimaji kwani wamepania kuendeleza kasi yao ili warudi kuongoza msimamo wa ligi.

Ili Azam iweze kujihakikishia kurudi kileleni ni lazima iiombee Yanga matokeo mabaya ya kufungwa au sare katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Stand United utakaopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles