25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Bocco arejea dimbani kuivaa Azam FC

MSHAMBULIAJI wa Simba,  John Bocco, huenda akaanza kucheza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 23 mwaka huu, Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Bocco alikuwa nje ya dimba kwa muda mrefu, baada ya kuumia nyama za paja, wakati aliichezea Simba mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam uliochezwa Agosti 17 mwaka huu, Uwanja wa Taifa,  Dar es Salaam.

Tatizo hilo lilimfanya kuwa nje ya dimba kwa zaidi kwa mwezi mmoja.

Hata hivyo katika mazoezi yaliyofanyika jana asubuhi Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa Simba alijifua na wachezaji  wengine wa kikosi hicho.

Ni wazi hiyo itakuwa habari njema kwa benchi la ufundi la Wekundu hao pamoja na mashabiki wa klabu hiyo, kwani mshambuliaji huyo amekuwa na mchango mkubwa kikosini kwao tangu aliposajiliwa kutoka Azam.

Bocco mbali ya kuwa mfungaji mzuri, pia amekuwa mtengenezaji mzuri wa mabao na wachezaji wengine na hasa mshambuliaji wa timu hiyo Meddie Kagere.

Simba ilirejea Dar es Salaam juzi jioni ikitokea Kigoma  ilikoenda kwa ziara ya kimichezo.

Ikiwa huko ilicheza  mechi mbili za kirafiki dhidi ya Mashujaa FC ya Daraja la Kwanza na kupata ushindi wa bao 1-0, kabla ya kuikabili Aigle Noir inayoshiriki Ligi Kuu Burundi na kutoka suluhu, mechi zote zilichezwa Uwanja wa Lake Tanganyika mkoanu humo.

Lakini kabla ya kutimkia Kigoma,  Simba iliumana na timu ya Bandari inayoshiriki Ligi Kuu Kenya na kushinda bao 1-0,  mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema leo watawapa mapumiziko wachezaji wao baada ya kutoka kwenye ziara ya Kigoma.

“Tumefanya mazoezi leo (jana) asubuhi lakini kesho hawatafanya,  tutawapa mapumziko na baada ya hapo wataendelea na programu ya mazoezi kama kawaida ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles