25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Bocco aiweka Yanga kiporo

Theresia Gasper-Dar es SAlaam

NAHODHA wa Simba, John Bocco, amesema kwa sasa macho yote kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam, kabla hawajaivaa Yanga Machi 8, mwaka huu.

Simba wanatarajia kucheza na Azam kesho mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Baada ya mchezo huo, Wekundu wa Msimbazi hao watavaana na Yanga Jumapili hii kwenye Dimba hilo la Taifa.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo wao juzi, Bocco alisema bado wana mchezo mgumu dhidi ya Azam ambao wamepanga kupata ushindi kabla ya kukutana na watani wao wa jadi, Yanga.

“Nafahamu tuna mchezo mgumu dhidi ya Yanga, lakini kabla ya hapo, tunakutana na Azam, mechi ambayo na yenyewe lazima tushinde, hivyo tutahakikisha tunapambana ili tuvune pointi tatu muhimu,” alisema.

Alisema kikosi chao kimeendelea kuonyesha mabadiliko makubwa katika mechi zao hivyo wataendelea kupambana ili waweze kupata ushindi kwa kila mchezo.

Bocco alisema timu hizo zinapokutana ushindani unakuaga mkubwa hivyo lazima wajipange kutofanya makosa yoyote ambayo yatawagharimu.

Mchezaji huyo aliendelea kusema ushindi lazima kwa timu hizo mbili pinzani ili waweze kupata pointi na kuendelea kujihakikishia kutetea ubingwa wao kwa mara nyingine.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles