23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Bobi Wine na wenzake watinga tena mahakamani

KAMPALA, UGANDA


MBUNGE wa Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina la Bobi Wine na wenzake zaidi ya 30 wamefikishwa mahakamani tena jana katika mji wa Gulu uliopo Kaskazini mwa nchi hii.

Kwa mujibu wa gazeti la New Vision la hapa, watuhumiwa hao 33 ambao walipewa dhamana baada ya kufunguliwa mashtaka ya ugaidi, walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Gulu kusomewa mashtaka yao.

Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kufanya mashambulizi dhidi ya gari la rais wakati wa kampeini za uchaguzi wa marudio katika Manispaa ya Arua, Septemba 15, mwaka huu.

Wabunge wengine wanaokabiliwa na tuhuma hizo ni Gerald Karuhanga (Ntungamo), Paul Mwiru (Jinja Mashariki) na Kassiano Wadri (Arua).

Mwingine ni Mbunge wa Mityana, Francis Zaake ambaye hakuwapo mahakamani ingawa mapema Septemba polisi walimwongezea kosa la uhaini na kutoroka akiwa chini ya ulinzi wao.

Hata hivyo wabunge hao waliachiwa kwa dhamana ya polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles