‘Blessing’ ya Babbi Music yaanza kusumbua

0
542

ARIZONA, MAREKANI

KUTOKA nchini Marekani , msanii wa Afro Pop mwenye asili ya Burundi, Babbi Music, amewashukuru mashabiki na vyombo vya habari Afrika Mashariki kwa kuipa nafasi video yake mpya, Blessing.

Akizungumza na MTANZANIA , Babbi alisema wimbo Blessing umekuwa gumzo zaidi huku mashabiki wengine wakidhani ameingia kwenye muziki wa gospo jambo ambalo sio la kweli.

“Blessing imekuja na baraka nyingi kwangu ikiwa ni pamoja na kupewa sapoti na vyombo vya habari karibia vyote hapo Bongo na nchi zingine za Afrika. Ni wimbo ambao unaweza kusikilizwa na kila mtu bila kujali imani yake na tayari video ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube,” alisema Babbi Music.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here