26.8 C
Dar es Salaam
Monday, December 6, 2021

Black Panther yajizolea tuzo Tatu Oscar

New York, Marekani

Tuzo za Filamu za Oscar (91st Oscars Annual Academy Awards) zimefanyika usiku wa kuamkia leo nchini Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali wanaofanya vizuri kwa sasa ulimwenguni.

Katika tuzo hizo Filamu iliyojizolea umaarufu mkubwa duniani ya Black Panther iliyochezwa na mastaa wengi akiwamo Mmarekani mwenye asili ya Kenya Lupita Nyong’o imeshinda tuzo Tatu.

Filamu hiyo imeshinda Tuzo ya Muandaaji Bora wa Filamu ambapo tuzo imeenda kwa waandaaji Jay Hart na Hannah Beachler, Filamu yenye mafanikio na Mbunifu Bora wa Mavazi ambayo imechukuliwa na Ruth Carter.

Hannah na Ruth ni wanawake wa kwanza weusi kushinda katika tuzo hizo kwenye vipengele vya Muandaaji na Mbunifu wa Mavazi.

Aidha katika vipengele vingine washindi na filamu walizocheza katika mabano, Muigizaji Bora wa Kiume ni Rami Malek (Bohemian Rhapsody), Muigizaji Bora wa Kike Olivia Colman (The Favourite), Mwanamuziki Lady Gaga ameshinda tuzo ya Wimbo Bora Asilia kupitia wimbo wake wa Shallow (A Star Is Born).

Washindi wengine ni Filamu Bora yenye Lugha ya Kigeni na Filamu yenye Picha Bora ambayo amechukua mpiga picha Alfonso Cuaron (Roma), Mahershala Ali kwa mara ya pili ameshinda kama muigizaji bora msaidizi (Green Book) na Katuni Bora Ndefu (Spider Man), Katuni Bora Fupi (Bao) na Makala Bora imeshinda (Period.End of Sentence).

Aidha tuzo hizo hufanyika kila mara nchini Marekani na mwanzoni zililalamikiwa kuwa na ubaguzi wa rangi kwa kutowapa tuzo wamarekani weusi lakini kila siku zilivyoenda waandaaji walibadilika na hivi karibuni wameshuhudiwa watu weusi wengi wakishinda tuzo hizo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,263FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles