BLACK PANTHER YAINGIZA BIL. 957/-

0
856

NEW YORK, MAREKANI


MKALI wa filamu nchini Marekani mwenye asili ya Kenya, Lupita Nyong’o, ameweka wazi kuwa filamu yao mpya ya Black Panther imeingiza dola milioni 427 kwa siku nne.

Filamu hiyo iliachiwa mapema mwezi huu, hivyo ndani ya siku nne iliweza kuuza mauzo ya jumla ya dola milioni 427 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 957.

Filamu hiyo kwa sasa inatikisa dunia kutokana na ubora wa stori yake, hivyo Lupita anafurahia mafanikio ya filamu hiyo.

“Tunashukuru filamu hii imekuwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa mashabiki, tunaamini ubora wake ndio kila kitu, ndani ya siku nne tangu kuachiwa imeweza kuingiza kiasi cha dola milioni 427, ni mafanikio makubwa,” alisema Lupita.

Bajeti ya kutengeneza filamu hiyo ilitajwa kuwa ni dola milioni 200 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 448, lakini kwa mauzo yaliyofanyika tayari fedha hiyo imerudi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here