29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Black Panther afariki dunia

IMAN MKETEMA

Tanzia: Staa wa filamu nchini Marekani, Chadwick Boseman (43) amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo kwa saratani ya utumbo aliyopambana nayo miaka minne sasa.

Booseman alijizolea umaarufu mkubwa alipocheza Black Panther, filamu iliyofanya mapinduzi kwenye mauzo na mpaka sasa imeingiza kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.3.

Licha ya Booseman kuigiza filamu ya Black Panther ni muigizaji aliyecheza sinema za kihistoria hapa ulimwenguni kama vile The Express: The Ernie Davis Story (2008), 42 (2013), Get on up (2013), Marshall (2017), Da 5 Bloods (2020).

Ndani ya Get On Up, Booseman alicheza kwa kuvaa uhusika wa mwanamuziki nguli wa soul marehemu, James Brown na akafanikiwa kuukumbatia umaarufu mkubwa.

Booseman ambaye amefariki nyumbani kwake akiwa mbele ya familia yake ataendelea kubaki kwenye mioyo ya watu kama mwigizaji wa kuigwa wa karne ya 21.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles