28.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Blac Chyna aionya familia ya Kardashian

NEW YORK, MAREKANI 

BIFU la mwanamitindo Blac Chyna na familia ya Kardashian, haliwezi kwisha baada ya mrembo huyo kuionya familia hiyo kutotumia jina la mtoto wake Dream katika kipindi chao cha runginga cha Keeping Up With The Kardashians.

Blac alipata mtoto huyo mwenye umri wa miaka miwili sasa wakati yupo kwenye uhusiano na Rob Kardashian, lakini baada ya kuachana mrembo huyo amekuwa na mgogoro na familia ya Rob kwa madai kijana wao hatoe huduma kwa mtoto huyo.

Hata hivyo Kim, Khloe, Kylie wamekuwa wakimzungumzia mtoto huyo wa kaka yao kwa namna tofauti, lakini Blac alianza kumuona Rob kuwa, aiambie familia yake iachane na mpango wa kumzungumzia mtoto wake.

Inasemekana kuwa Blac na yeye anataka kuwa na kipindi chake cha runinga ambacho kitakuwa kinajulikana kwa jina la The Real Blac Chyna, hivyo hayupo tayari kuona mtoto wake akizungumziwa kwenye vipindi vingine.

“Vipindi vingine vinafanya vizuri kutokana na kutaja majina ya watu, Keeping Up With The Kardashians sitaki kuona wakimzungumzia mwanangu,” alisema Blac.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,085FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles