Blac akamatwa na dawa za kulevya

0
680

BlacTEXAS, MAREKANI

ALIYEKUWA mke wa msanii wa hip hop nchini Marekani Tyga, Blac Chyna, amekamatwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Austin Bergstrom uliopo mjini Texas nchini Marekani akiwa na dawa za kulevya.

Mrembo huyo mwenye mtoto mmoja, amekamatwa kwenye uwanja huo akiwa anaelekea London nchini England akiwa na dawa hizo.

Inasemekana kuwa alifanikiwa kupita uwanjani hapo lakini alikuja kukamatwa kwenye mlango wa ndege baada ya mlango huo kupiga kelele kuashiria kitu tofauti ndipo aliposachiwa akakutwa na dawa hizo.

Chanzo cha habari kiliieleza TMZ kwamba, mrembo huyo alijaribu kupambana na mhudumu wa ndege hiyo lakini alishindwa baada ya mhudumu mwingine kutokea na kumkaba hadi sasa anashikiliwa na polisi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here