22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Biteko: Waliokataa fidia zao Tarime wakazichukue kwenye halmashauri

Anna Potinus

Waziri wa Madini, Dotto Biteko amewataka wananchi wa Tarime waliokataa fidia zao walizopewa kutokana na kubomolewa nyumba zao kuhakikisha wanaenda kuchukua hundi zao katika halmashauri ya wilaya hiyo.

Biteko ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumanne Novemba 5, alipokuwa akijibu swali na nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Agnes Marwa lililokuwa na vipengele viwili ambapo amehoji ni lini Mgodi wa Accacia uliopo Nyamongo wilayani Tarime utalipa fidia za wananchi hao.

“Wananchi wengi wamebomolewa nyumba zao na mgodi wa Accacia na wengine hawajalipwa fidia hadi sasa aidha mgodi pia umeanza kuchimba madini kwenye maeneo ya watu, je ni lini mgodi huo utalipa fidia za watu hawa.

“Kutokana na shilingi kupanda thamani kila mwaka na vifaa vya ujenzi kupanda thamani kila mwaka, deni la wananchi wa Nyamongo wanaodai fidia sasa imekuwa ni muda mrefu je watakapowalipa hizo fedha watawalipa na fidia kutokana na ukweli kuwa na wao wana familia na mahitaji yao ambayo yamesimama baada ya kuondolewa katika maeneo yao,” amehoji.

Akijibu swali hilo, Biteko amesema serikali imeendelea kusimamia sekta ya madini kwa kuhakikisha uwekezaji unafanyika kwa kuzingatia sheria za nchi na taratibu za nchi ikiwemo kuhakikisha wananchi wanaoishi katika maeneo ambayo miradi ya uendelezaji migodi inataka kufanyika na kulazimika kupisha maeneo yao wanalipwafidia stahiki na wanapewa makazi mbadala kuliko waliyokuwa nayo awali.

“Ziko fidia ambazo fedha zilishatolewa muda mrefu lakini bahati mbaya hazijalipwa kwa wananchi na ni kwasababu kuna wananchi baada ya kulipwa walikataa hivyo zikawekwa kwenye halmasahauri kwahiyo ninadhami sio sahihi kuupa mzigo tena mgodi kwamba walipe na fidia kwa sababu fedha hazijachukuliwa.

“Wale wananchi waliozikataa mwanzo walikuwa ni 138, waliochukua hundi ni 70 wakabaki 64, hivyo niwaombe wakazichukue cheki zao kwasababu fedha zao ziko pale kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Tarime,” amesema Biteko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles