27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Biteko awataka maofisa madini kuwa waadilifu

 MWANDISHI WETU -ARUSHA

WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko amewataka maofisa madini wa mikoa kuwa waadilifu katika kazi zao huku wakiepuka utoaji wa taarifa zisizo na usahihi kwa umma ili kuwaepusha migongano ya taarifa kwa wananchi.

Biteko ameyasema hayo wakati akizungumza na maofisa hao wa mikoa katika mkutano wa mwaka wa maofisa madini mikoa wa majumuisho kati ya menejimenti ya wizara na Tume ya Madini uliofanyika jijini Arusha hivi karibuni.

Alisema kuwa mwaka wa fedha uliopita wizara ilikadiria kukusanya mapato yatokanayo na madini ya zaidi ya Sh bilioni 470 ambapo ilifanikiwa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 528 sawa na asilimia 12.3

Aidha alisema ni vyema maafisa madini wakafuata sheria ili kuepuka migogoro kwani wanaishi na jamii ya wafanyabiashara wa madini wanaotaka faida ya haraka hivyo wahakikishe taarifa za uongo au ukweli zinazokuja ofisini kwao wazifanyie kazi bila kumuonea mtu.

“Msinunue migogoro ya watu kwani mkuu wa wilaya amepewa uhalali katika eneo lake la kiutawala na kufanya uamuzi wa kitu ukakosea kidogo lakini haupati uhalali wa wewe Ofisa Madini kumkosoa hivyo ni vyema akapeleka malalamiko katika ngazi ya katibu tawala mkoa kwa ajili ya usuluhishi,” alisema Biteko

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila alimuelekeza Katibu Mtendaji wa Tume na Kamishna wa Madini wakae pamoja na kupitia namna ya kutekeleza au kutafuta usuluhishi wa mapendekezo yao pamoja na kuandaa taarifa itakayoonyesha ni kwa namna gani watayatekeleza ili maafisa madini mikoa waweze kupata taarifa na kusaidia namna ya kutekeleza pale watakapohitajika.

Ameongeza kuwa kufuatia utekeleza mzuri katika sekta ya madini kumepelekea kuongezeka kwa bajeti ya wizara ya mwaka 2020 kwa milioni 11.

“Sasa hivi natembea kifua mbele kwani mlinituma kukusanya bilioni 470 nimekuletea bilioni 528 sasa niongeze nyingine nikakusanye nyingi zaidi na ndiyo maana bajeti ya wizara ya mwaka huu imeongezeka kwa sababu ya mafanikio hayo,” alisema Msanjila

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idrissa Kikula alisema kuwa moja ya majukumu ya tume ni kukusanya maduhuli pamoja na kutatua migogoro hivyo yanapaswa kutendewa kazi kwani sekta ya madini inakuwa kwa asilimia 17 hivyo kila mmoja ajiweke sawa kuhakikisha asilimia hizo zinapanda na kufikia asilimia 20 ili kuweza kupandisha hadhi sekta ya madini.

Sambamba na hayo aliwahimiza maofisa hao kuendelea kuhakikisha malengo ambayo wamepewa na uongozi wanayatekeleza ili kuweza kilinda hadhi na heshima ya wizara kwa kuwahamasisha wengine kuweza kufanya kazi kwa bidii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles