23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Biteko ajadili changamoto za barabara

Na Tito Mselem -Geita

WAZIRI wa Madini, Doto Biteko, ameshiriki kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Geita kujadili changamoto za barabara mkoani humo.  

Kikao hicho kilifanyika jana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na CCM na wabunge wa mkoa huo.

Katika kikao hicho, Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Bukombe, aliwapongeza viongozi wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Geita na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) kwa kazi nzuri waliyofanya kuhakikisha kuwa barabara zinatengenezwa kwa kiwango kizuri na kumalizika kwa wakati.

Biteko alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri katika kuhakisha barabara za mkoa huo zinakamilika kwa muda uliopangwa na zinakuwa kwenye viwango vinavyotakiwa.

Imeelezwa kuwa Geita ni kati ya miji inayokua kwa kasi sana sambamba na ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi, hivyo kuwepo na msongamano mkubwa wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu barabarani. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita, Gabriel alisema Serikali ya Rais Dk. John Magufuli ilitoa ahadi ya barabara na imetekeleza kwa wakati.

“Alitupa ahadi ya ujenzi wa barabara na ametekeleza ujenzi wa Barabara ya Ushirombo mpaka Lusahunga kilometa 110 kwa gharama ya Sh bilioni 114.557, Uwanja wa Ndege wa Chato kilometa 3.5 kwa gharama ya Sh billioni 39.15.  

“Kazi ambazo zimekamilika ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Runzewe mpaka Bwanga kilometa 45 kwa gharama ya Sh bilioni 43.357 na Barabara ya Bwanga mpaka Biharamulo kilometa 65.0. Miradi yote hii inatekelezwa kwa fedha za Serikali,” alisema. 

Katika hatua nyingine, Gabriel alisema katika Mkoa wa Geita, Tanroads inasimamia miradi ya usanifu wa kina katika barabara ya Geita hadi Kahama yenye kilometa 139.557 kwa gharama ya Sh bilioni 440 inayotelekezwa na mkandarasi ENV Engeneering na kazi imekamilika. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles