33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Binti mwenye asili ya Somalia anayemvuruga Rais Trump

HASSAN DAUDI Na MITANDAO

HATA miezi saba haijapita tangu alipoingia bungeni, lakini mwakilishi huyu wa wananchi wa Minnesota kupitia Chama cha Republic, bibiye Ilhan Omar, amekuwa mwiba mchungu kwa Rais wa Marekani, Donald Trump.

Haya yanakuja wakati ikiwa imebaki miezi michache kuelea Uchaguzi Mkuu wa mwakani, ambapo Rais Trump anakabiliwa na kibarua cha kumaliza awamu ya pili madarakani baada ya ile ya kwanza ya miaka minne.

Unaweza kujiuliza kwanini mwanamke huyo anaweza kumpasua kichwa Rais Trump? Jibu ni kwamba kitendo cha Ilhan kukulia Minessota ni tatizo kubwa endapo wananchi wa eneo hilo watamuunga mkono na kumpa kisogo Rais Trump katika uchaguzi wa mwakani.

Ni kwa sababu eneo hilo linasifika kwa kuwa na wakazi wengi wenye asili ya Somalia na kwa sababu hiyo, limepewa jina jipya na wananchi wa Marekani, likifahamika kwa jina la ‘Mogadishu Ndogo.’

Hiyo ni baada ya kile kilichotokea siku chache zilizopita, ambapo Rais Trump alimshambulia kwa maneno mbunge huyo, kauli ambazo zilitafsiriwa kuwa ni za kibaguzi.

Wengi wanatambua kuwa Ilhan amekuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wa Rais Trump tangu alipoingia madarakani kuiongoza Minnesota kupitia Uchaguzi wa mwaka huu, akijitambulisha kwa jina la ‘tatizo kwa Rais (Trump)’.

Alichokisema Rais Trump, ambacho ndicho kilichoibua sekeseke lililopo sasa, ni kwamba Ilhan mzaliwa wa Somalia, na wabunge wengine wanne wa Republican, akimaanisha Alexandria Ocasio-Cortez wa New York, Ayanna Pressley (Massachusetts) na Rashida Tlaib (Michigan) wanapaswa kurejea kwao, maeneo aliyoyataja kuwa yamejaa matukio ya kihalifu.

Kati ya hao, Ilhan alikuwa wa kwanza kujibu mapigo, akisema kauli ya kiongozi wao huyo wa nchi ni ishara ya vitendo vya ubaguzi na inapaswa kupigwa vita kwa kuwa walichaguliwa na wananchi kuingia bungeni.

Aidha, Jumatano ya wiki hii, Rais Trump akiwa North Carolina, hakuweza kujizuia kutoa kauli iliyoonekana wazi kuwa ni ya chuki dhidi ya Ilhan, akimtaja kuwa ni mdau wa kikundi cha kigaidi cha Al Qaeda.

Huenda unajiuliza sababu ya Rais Trump kumganda mwanamke huyo. Japo ni ngumu kuthibitisha, lakini wengi wanaamini kuwa ni kwa sababu Ilhan ndiye mwanamke pekee kati ya wale wanne, aliyezaliwa nje ya Marekani.

Kilichomfanya mwanamke huyo kuwa Marekani leo hii, hata kuingia bungeni ni kukimbia vita za wenyewe kwa wenyewe nchini kwao, Somalia.

Lakini pia, wachambuzi wa sisasa za kimataifa wanatambua wazi kwamba kinachomfanya Ilhan kuwa adui mkubwa mbele ya wapambe wa Rais Trump ni kauli zake juu ya Iran, moja kati ya mataifa yanayoungwa mkono na Marekani.

Akiwa muumini mzuri wa Dini ya Kiislamu, mara nyingi amekuwa akitumia kurasa zake za mtandao wa Twitter kuonesha kutofautiana na sera zote za Marekani zinazoliunga mkono Taifa la Iran.

Kulithibitisha hilo, ni kile alichowahi kukieleza katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Tweeter mwanzoni mwa mwaka 2012, alipoandika: “…Allah (Mungu) wazindue watu kwa uovu unaofanywa na Israel.”

Licha ya kwamba aliomba msamaha baadaye, kauli yake ya kuwa wanasiasa wengi wanaounga mkono kila kinachofanywa na siasa, huvutwa na ushawishi wa fedha na si kweli kwamba wana mapenzi dhidi ya nchi hiyo, inaonesha wazi kuwa Ilhan ni adui wa sera za chuki dhidi ya Israel, jambo ambalo moja kwa moja linamfanya kuwa adui wa Rais Trump.

Lakini pia, ukiliweka kando hilo la Israel, unaweza kuona chanzo cha Rais Trump kumchukia mwanasiasa huyo ni kikundi cha ugaidi cha Al Qaeda.

Tuanzie na kile alichokisema katika Baraza la kujadili uhusiano wa Marekani na mataifa ya Kiislamu, ambapo Ilhan alilizungumzia tukio la shambulio la kigaidi la Septemba 11 na kauli yake kutajwa kuunga mkono kile kilichofanyika. Anasema: “Watu fulani wamefanya kitu (kizuri).”

Wengi kati ya wafuasi wa Rais Trump, ambao moja kwa moja ni maadui wa Al Qaeda, wanaamini mwanasiasa huyo ni mdau wa magaidi na wala hakuumizwa na tukio hilo lililopoteza maisha ya watu takribani 3,000.

Hata hivyo, wakati Rais Trump akimuona Ilhan kuwa adui, ieleweke kuwa wapo wanaomuunga mkono mwanamke huyo mwenye umaarufu mkubwa kwa uhasimu wake na kiongozi huyo.

Wakati huo huo, miongoni mwa wanaomuona Ilhan kuwa wa maana zaidi kuliko Rais Trump ni mgombea anayepewa nafasi kubwa ya kuukwaa urais wa Marekani katika Uchaguzi wa mwakani kupitia Chama cha Democratic, Bernie Sanders, ambaye anamtaja bila woga kiongozi huyo wa nchi kuwa ni mbaguzi.

Sambamba na Sanders, Seneta wa California, Kamala Harris, anamuona Rais Trump kuwa ni mwenye nia ya kuligawa taifa hilo lenye nguvu kubwa kiuchumi duniani, kile ambacho pia kimetajwa na Seneta wa Massachusetts, Elizabeth Warren.

Changamoto kubwa aliyonayo Rais Trump ni kwamba bado si wengi kati ya wanasiasa wa chama chake, Republicans, waliotayari kujitosa moja kwa moja katika uhasimu wake na mwanasiasa huyo wa kike.

SAFARI YA ILHAN OMAR KISIASA

Mwanasiasa huyu wa nchini Marekani alizaliwa Oktoba 4, 1981 nchini Somalia.

Alizaliwa katika mji wa Mogadishu na kulelewa Baydhabo, Somalia.

Baada ya vita kuzuka nchini Somalia mwaka 1991, familia yake ilitoroka na kukimbilia katika kambi ya wakimbizi nchini Kenya.

Alifuzu katika Chuo Kikuu cha North Dakota State, alikokuwa akisomea Sayansi ya Siasa na masuala ya kimataifa, mwaka 2011.

Ilhan alichaguliwa kupitia Chama cha Democtratic, mwaka 2016, kuwa mwakilishi katika Bunge la Wawakilishi Jimbo la Minnesota, na kuweka historia ya kuwa mbunge wa kwanza wa raia wa Marekani, mzaliwa wa Somalia kuchaguliwa kwenye nafasi za uongozi Marekani.

Mwanamke huyu jasiri, ni mkurugenzi wa sera na miradi ya mtandao wa wanawake. Na sasa amechaguliwa katika Bunge la Wawakilishi nchini Marekani.

Anaeleza kuwa kuna umuhimu mkubwa na kwamba inaleta matumaini kuwa mwanamke wa jamii ya Kisomali, anayevaa hijjab kuapishwa akiwa ameshikilia msahafu au Qur-an kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles