26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Bima ya afya kutolewa nyumba kwa nyumba

AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

MFUMO wa vifurushi vya Bima ya Afya umezinduliwa rasmia jana jijini Dar es Salaam, huku Mwenyekiti wa Bodi ya Mfumo wa Bima ya Taifa (NHIF) Anna Makinda, akisema watu watafuata mpaka majumbani kupewa elimu ili wajiunge.

Makinda ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge, aliwataka pia watumishi wa vituo vya afya na hospitali, kuwa na lugha nzuri kwa watu wanaotumia bima hizo.

Alisema kuna baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa hawatoi kipaumbelea kwa watu wanaotumia bima ya afya na kuwataka waache tabia hizo.

“Utoaji wa huduma za afya sasa unaenda kwa ushindani, hospitali yenye wahudumu wa afya wanaotoa huduma nzuri ndio watakaopata fedha nyingi, mtu akiumwa atatamani kwenda kwenye hospitali inayotoa huduma nzuri.

“Wahuduma waendelee kuwa na bidii, kuna baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa na lugha chafu kwa wagonjwa hasa wanaotumia bima, hawa nawaambia waache tabia hiyo wagonjwa, wanahitaji lugha zenye faraja.

“Uzinduzi huu unaenda na ile azima ya Tanzania ya viwanda, utakuwa na msaada katika kuleta  afya njema kwajamii kwani bila afya njema hakuna uchumi wa viwanda, hivyo ni msaada mkubwa kwa wananchi wote, watumishi watapita majumbani kutoa elimu ya vifurushi hivi ili watu wengi wajiunge,”alieleza Makinda.

Kutokana na baadhi ya watu kuamini kuwa kukata bima ni kupoteza fedha, Makinda aliwaomba Watanzania waweke kipaumbele katika kupata bima ya afya kwa hiyari ili kuepuka gharama kubwa wanapougua.

“Afya ni kitu cha kwanza, kama huna afya njema hata kufanya kazi huwezi, hivyo watu wakate bima kabla ya kuugua, si mtu anaugua halafu anaenda hospitalini akitajiwa gharama ndo anataka akakate bima, mwanzo kuna watu walikuwa wanadanganya kuwa wako kwenye vikundi lakini hawapo sasa mfumo huu unaruhusu mtu mmoja mmoja, watu wabadilishe mtazamo kuwa wasipoumwa watapoteza fedha, nasisitiza mkate bima,” alisema Makinda.

Alisema Serikali itaendelea kuboresha hospitali za chini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa ukaribu na kupunguza msongamano katika hospitali ya rufaa.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Wizara ya Afya, Grace Magembe, alisema lengo la mfumo huo  ni mkakati wa kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza  kutokana na kuwepo kwa huduma za kibingwa ndani ya nchi.

 “Huduma za kibingwa katika hospitali zetu zinaendelea kuongezeka, Serikali inaendelea kuwekeza katika afya hivyo kupitia bima ya afya kila mtu atakuwa na uwezo wa kupata huduma bora  hata kama niwa kipato cha chini,”alieleza.

 Naye Mkurugenzi wa NHIF, Bernard Konga, alisema wataendela kuboresha vifurushi hivyo ili watumiaji waweze kulipia vifurushi hizo kwa awamu kwa njia ya benki na mitandao ya simu mpaka malipo yatakapokamilika.

“Huu ni mpango wa hiari utapatikana katika ngazi zote hospitali za serikali,binafsi na za taasisi za dini, utaratibu huu ni wa mtu binafsi si lazima awe kwenye taasisi, hata hivyo bado tunaendelea na majadiliano na taasisi ya fedha na mitandao ya simu ili kupunguza huu mzigo maana wengi wanasema kulipa kwa siku moja ni gharama zaidi hivyo tuanzisha mfumo wa kudunduliza.

“Tutaenda kila mkoa kutoa hamasa ya matumizi ya bima, huko mbeleni tunataka tufanye bima ya afya kuwa ya watu wote hivyo kwanza sahivi tunaanza kwa hiyari, kwenye nchi nyingine bila bima afya huwezi kutibiwa hivyo watu wazingatie hili,”alisema.

Vifurushi vya bima vilivyo zinduliwa ni vya aina ni Najali Afya, Wekeza Afya na Timiza Afya

Katika vifurushi hivyo mtu mmoja kuanzia miaka 18 hadi 35 atachangia Sh 192,000 kwa kifurushi cha Najali Afya ,384,00 kwa kifurushi cha Wekeza na 516,000 kwa kifurushi cha Timiza .

 Katika vifurushi hivyo mtu wa kuanzia umri wa miaka 36 hadi 59 atachangia Sh 240,000 kwa kifurushi cha Najali, Sh 444,000 kwa kifurushi cha Wekeza, na Sh 612,000 kwa kifurushi cha Timiza kwa mchangiaji wa miaka 60 na kuendelea atachangia Sh 360,000 kwa Najali, Sh 660,00 kwa Wekeza na Sh 984,000 kwa Timiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles