29 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Bilo atamba kuendeleza rekodi dhidi ya Simba, Yanga

Mohammed Kassara -Dar es salaam

KOCHA Mkuu wa Alliance FC, Athuman Bilal ‘Bilo’, ametamba kuendeleza rekodi zake za kuzipa wakati mgumu timu kongwe za Simba na Yanga, wakatakapokutana nazo katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Bilo alikiongoza kikosi cha Stand United kuvuna pointi tatu muhimu katika mchezo wa ligi hiyo msimu uliopita dhidi ya Yanga, baada ya kuichapa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa Januari 19, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Si Yanga pekee, kocha huyo pia aliwahi kuiwezesha timu hiyo kuigomea Simba kuvuna pointi zote tatu baada ya kuilazimisha sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa  Machi 2, mwaka jana, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Bilo alisema licha ya kuhamia makazi mapya, atahakikisha anakifanya kikosi chake hicho kuwa mwiba mchungu kwa vigogo hao wa soka kila watakapokutana.

“Nina furaha kuanza maisha mapya ndani ya Alliance, ni moja ya timu nzuri nchini kutokana na vijana walionao, pia sera yao ya kuweka msingi katika soka la vijana ni moja ya sababu kubwa itakayofanya tufanye vizuri msimu ujao.

“Mimi ni muumini mkubwa wa soka la vijana na kwa wachezaji nilionao, wakipata muda kidogo wa kuzoean, tutatisha. Lengo langu ni kuhakikisha naendeleza rekodi zangu nzuri dhidi ya Simba na Yanga, hawatachukua pointi tatu kwetu, ninataka Alliance iwe mwiba mchungu kwa vigogo hao msimu ujao,” alisema Bilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles