27.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Bility akata rufaa ya kumzuia kuwania urais FIFA

Musa BilityZURICH, USWIS

RAIS wa Shirikisho la Soka la Liberia, Musa Bility, amekata rufaa kwenye mahakama ya kutatua mizozo ya michezo (Cas), kwa kumzuia kugombea urais wa Shirikisho la Soka Duniani, Fifa.

Rais huyo alizuiwa kuwania kugombea nafasi hiyo na kamati ya uchaguzi ya Fifa kwa madai kwamba hakupita vigezo vya maadili.

Hata hivyo, Bility ameishangaa kamati hiyo kwa maelezo yake ambapo amedai kuwa haijatenda haki, ila kutakuwa na mipango ambayo imepangwa ili kutaka kumharibia.

“Uamuzi wa Kamati ya Fifa si wa haki, unaudhi na kusikitisha, hata hivyo, nimekata rufaa kwa CAS nikiwahimiza washughulikie rufaa yangu kwa dharura.

Bility, mwenye umri wa miaka 48, amekosoa uhalali wa vigezo vilivyotumiwa na pia ameitaka Fifa kuweka wazi matokeo ya uchunguzi kuhusu kila mgombea kwa mashirikisho yote 209 ya soka.

“Wanatakiwa kuweka wazi kila jambo kwa wagombea wote kutokana na uchunguzi wanaoufanya, kwa upande wangu niko tayari kuchunguzwa, lakini naona hawako wazi, wanafanya mambo kwa sir,i hivyo wataharibu utaratibu wa uchaguzi,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles