33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni moja kusaidia watoto wa kike halmashauri nane Mwanza

Mwandishi Wetu, Mwanza

Kiasi cha Sh bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwa mtoto wa kike ndani ya halmashauri nane za Mkoa wa Mwanza.

Huduma hizo ambazo zinazotolewa ni pamoja na elimu ya kujitambua kwa mtoto wa kike na ujasiriamali, chini ya mradi wa Msichana Dhabiti.

Akizungumza na Mtanzania Digital ofisini kwake, meneja miradi wa asasi ya kiraia ya Amani Girls, Revocatus Sono amesema mradi huo wa miaka mitatu, unalenga kuwafikia wasichana wa kati ya miaka 10 hadi 19 ambao wapo shuleni na wale waliohitimu.

Amesema fedha hizo ni ufadhili kutoka shirika la Novo Foundation la nchini Marekani kupitia shirika la Tides linalosimamaia ugawaji wa fedha hizo.

“Fedha hizo zinakuja kwa mafungu, kwa mwaka tunapokea Sh milioni 337.5. Ziko asasi 17 ambazo wote tunatarajia kupata ruzuku ya fedha hiyo,” amesema Sono

Aidha amesema asasi ya Amani Girls, kwa Tanzania itakuwa mratibu wa fedha inayotumwa ili kuhakikisha inatumika ipasavyo.

Naye Mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya Fadhili Teens Tanzania (FTT), Athanas Evarist amesema wamelenga watoto wa kike kutokana na kundi hilo kuwa sehemu kubwa ya watu wanaopitia dhuluma nyingi lakini pia kwenda na sera ya taifa ya Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (Mtakuwwa).

“Kwa mfano sisi, FTT tayari tuna miradi mbalimbali inayowahusu watoto wa kike. Wilayani Sengerema tuna mradi unaitwa Msichana Initiative wakati wilayani Magu, tuna mradi unaitwa Binti Mwerevu. Hii ina maana kwamba kila asasi ina sera zake za namna ya kutekeleza miradi yao,” amesema Evarist

Mradi wa Msichana Dhabiti, umezinduliwa Agosti Mosi, 2019 na unatarajiwa kumalizika Agosti Mosi 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles