26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, January 27, 2022

Bilioni mbili za Makonda kwa wasanii kutoka Machi

Anna Potinus – Dar es Salaam

Msanii wa Filamu za Bongo, Steve Nyerere amesema kwamba safari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya wasanii kwenda kutembelea mradi wa ujenzi wa reli, Standard Gauge suala hilo sio la kisiasa bali ni la utekelezaji wa miradi mikubwa kwa manufaa ya Watanzania.

Ametoa tamko hilo leo Februari 5, 2019 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wasanii jijini Dar es Salaam ambapo amesema safari hiyo itaanza Februari 7, 2019.

“Tunaenda kule kuangalia mradi ulipofikia maana kuna wengine watasema tunaendaje wakati sio wataalamu wa mambo hayo, kila makundi yatajipanga kwa nafasi zao sisi kama wasanii tumeiona fursa tunakwenda kuangalia mradi huo,” amesema.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa ahadi iliyotolewa na Makonda ya kutoa mikopo kwa wasanii bado ipo na mwezi Machi kiasi cha shilingi bilioni mbili zitakuwepo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa na yeyote mwenye mradi wake atakopeshwa.

“Bilioni mbili zipo tayari na kuanzia Machi wasanii wote wanaweza kwenda kuchukua mkopo na sio kwa watu maarufu tu kama Khadija kopa bali hata waandishi wa habari wanayo nafasi ya kupata mkopo huo,” amesema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,866FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles