29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

BILIONI 5/- KUGAWIWA WATEJA WA TIGO

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


TigoKAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo, imetangaza gawio jingine la malipo ya faida ya robo mwaka la Sh bilioni 5.82 ambalo litagawiwa kwa wateja wote wanaotumia huduma ya fedha kupitia simu.

Gawio hilo ni la kipindi cha robo ya nne ya mwaka ulioishia Desemba 31, 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Huduma za Fedha kwa simu wa Tigo, Ruan Swanepoel, alisema kampuni hiyo kwa ujumla imeshawalipa wateja wake wanaotumia huduma za fedha kwa njia ya simu jumla ya Sh bilioni 5.82, sawa na Dola za Marekani milioni 26.3 kama malipo ya robo mwaka tangu kuanzishwa malipo hayo ya riba na Tigo Julai 2014.

Alisema katika robo ya kwanza ya mwaka, riba iliyotolewa kama gawio ilipanda hadi asilimia 11 ikiwa ni matokeo mazuri ya viwango vilivyopokelewa katika mfuko wa fedha uliowekwa katika benki mbalimbali za biashara nchini.

“Riba hii ni malipo kwa wateja binafsi, mawakala wa rejareja, mawakala wakubwa na wabia wengine wa kibiashara wa Tigo ambao kila mmoja anapokea malipo kulingana na thamani ya fedha zilizohifadhiwa katika pochi ya kielektroniki ya Tigo pesa,” alisema Swanepoel.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Tigo, Christopher Kimaro, alisema kuongezeka kwa faida kumetokana na kuboreshwa kwa mazingira ya soko na kasi ya kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa Tigo pesa kama kichocheo kikubwa katika ongezeko kubwa la gawio la riba hususani kwa upande wa wafanyabiashara.

Alisema Tigo pesa kwa sasa ina mtandao mkubwa wa wafanyabiashara zaidi 55,000 wanaowezesha malipo ya miamala nchini kote.

“Tigo pesa inakuwa ni huduma ya kwanza ya fedha kwa njia ya simu duniani ambayo mwaka 2014 iligawa gawio la hisa lililoanzishwa kutoka katika akaunti ya dhamana ya fedha katika simu katika mfumo wa gawio la robo mwaka kwa wateja,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles