28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

BILIONI 46 ZAPUNGUA BAJETI YA WAZIRI MKUU, BUNGE LAONGEZA BILIONI 3.8

Fredy Azzah, Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi yake na Mfumo wa Bunge kwa mwaka 2018/19, inayoonyesha bajeti yake imepungua kwa Sh bilioni 46.7 huku ya Bunge ikiongezeka kwa Sh bilioni 3.87.

Akisoma hotuba yake bungeni mjini Dodoma leo Jumatano Aprili 4, Waziri Mkuu Majaliwa ameomba Bunge kuidhinishiwa Sh bilioni 124.954 kati yake Sh bilioni 66.162 ni matumizi ya kawaida na Sh bilioni 58.791 ni matumizi ya maendeleo.

Pia ametaka Bunge kuidhinisha Sh bilioni 125.521 kwa ajili ya Mfuko wa Bunge kati yake Sh bilioni 117.205 kwaajili ya matumizi ya kawaida na Sh bilioni 8.315 matumizi ya maendeleo.

Katika mwaka wa fedha utakaoisha Juni 31, Ofisi ya Waziri Mkuu iliomba kuidhinishiwa Sh bilioni 171.66 huku Ofisi ya Bunge ikiidhinishiwa Sh bilioni 121.65.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles