26.8 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni 17 kutumika kujenga soko jipya la Kirumba

Na Sheila Katikula,Mwanza

Serikali inatarajia kuanza kujenga soko la kisasa la Kirumba jijini Mwanza litakalokuwa na ghorofa moja kwa gharama ya Sh bilioni 17.

Mwenyekiti wa soko la Kirumba, Elias Daud.

Hayo yamesemwa Julai 25, 2022 na Diwani wa Kirumba, Wessa Juma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake nakubainisha kuwa ujenzi huo wa soko utafanyika ndani ya mwaka mmoja pamoja na barabara zinazozunguka soko hilo zenye urefu wa kilometa 2.9.

“Benki ya Dunia imetoa mkopo wa Sh bilioni 17 kwa ajili ya maendeleo ya kata yetu tunatarajia kuanza ujenzi wa soko la kisasa la ghorofa moja na barabara za kilometa 2.9 zinazozunguka soko hili.

“Ujenzi utakapoanza kila Mfanyabiashara ambaye amejiandikisha na amepigwa picha atapewa nafasi ya kufanyia biashara,” amesema Juma.

Amesema wafanyabiasha wa soko hilo wanaotarajiwa kuhamia kwenye uwanja wa magomeni ili kupisha ujenzi unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

“Kuna taratibu zinaendelea za kuwahamisha wafanyabiasha hawa ili waweze kupisha ujenzi huu kwani tume jenga vyoo vya matundu sita, huduma ya maji na umeme imekamilika wakati wowote watahama kwenye soko hili,” amesema Juma.

Hata hivyo, amewataka wafanyabiashara hao kuondoa hofu ya kupoteza wateja wao kwa sababu ya kuhama kwa soko hilo kwani magomeni ni sehemu salama na inafikika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa soko la Kirumba, Elias Daud amesema soko hili lina wafanyabiashara 650 wameanza kupewa maeneo ili waweze kuhamia soko jipya na kupisha ujenzi.

“Ujenzi wa soko la muda la magomeni unaendelea tupo katika hatua za kuezeka vyumba vya maduka na kupima maeneo ya wafanyabiasha wadogo, tumekubaliana na serikali tujenge hapa kwenye uwanja huu kwa fedha zetu na soko jipya likikamilika tutabomoa hapa na kupaacha wazi kama tulivyopakuta.

“Wafanyabiashara wanatakiwa kuondoa hofu kuhusu wateja sababu wateja wanaonunua kirumba ndio hao hao watakaokuja kununua magomeni maana tunahama na biashara Zetu na tunahama wote kwa pamoja,” amesema Daud.

Aidha, ameishukru serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga soko hilo kwa sababu miundo mbinu yake siyo rafiki.

Wakizungunza kwa nyakati tofauti, wafanyabiashara wa soko hilo, Ashura Juma na Mohamed Ally wameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kujenga soko la kisasa hali ambayo itasaidia kuongeza Pato la taifa na kuwanufaisha wafanyabiashara kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles