20.5 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Bilioni 100 kusambaza umeme mitaa inayofanana na vijiji

Hadija Omary, Lindi

Serikali kupitia Wizara ya Nishati, imetenga Sh 103.8 kwa ajili ya kusambaza umeme  kwenye mitaa inayofanana na vijiji mkoani Lindi.

Hayo yameelezwa na waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani juzi wakati wa uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa miundobinu ya gesi asilia majumbani mkoani Lindi uliofanyika katika Kata ya Mnazi Mmoja  Manispaa ya Lindi.

Kalemani amekiri kuna maeneo ya mjini ambayo mengi yaliitwa kama mitaa na si vijiji wakati kuna mitaa ambayo haina tofauti na vijiji.

“Tumeshatoa maelekezo kuwa mitaa yote inayofanana na vijiji iwe kwenye miji, Manispaa ama majiji yote ipelekewe umeme kwa Sh 27,000,” amesema.

Aidha, amesema fedha hizo zimetengwa katika bajeti ya mwaka 2019/2020 huku akimsisitiza Meneja wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Kanda ya kusini, Feisian Makota kuzingatia na kuanza kutekeleza maagizo hayo kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

Awali akimkaribisha Waziri wa Nishati kuzungumza na wananchi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alimuomba waziri huyo kuangalia namna ya kuwaunganisha wananchi wanaoishi katika maeneo hayo sawa na wale wa vijijini ambako miradi ya REA inatekelezwa.

Zambi alisema kuna baadhi ya mitaa ndani ya manispaa hiyo ipo vijijini ambayo kuna haja ya Serikali kuwaangalia wananchi wa maeneo hayo walipie malipo ya umeme sawa na yale yanayofanywa na wananchi wa vijijini ambako miradi ya REA imefika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles