28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Bilioni 1.8 zatumika kuendeleza wasichana 1,269 kielimu Muleba

Renatha Kipaka, Muleba

Zaidi ya Sh Bilioni 1.8 zimetumika kuwasaidia mabinti 1,269 wenye umri wa miaka 14 na kuendelea kuwapeleka katika Vyuo vya Ufundi kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

Wasichana hao walishikwa mkono na Shirika lisilo la Kiserikali la Humuliza la wilayani Muleba mkoani Kagera lengo likiwa nikuwasaidia kutimiza ndoto zao pamoja na kupata ujuzi utakaowasaidia kupata kipato ili kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Humuliza, Victor Nestory lililopo katika kijiji cha Bunyagongo kata ya Nshamba wilayani humo, wakati akizungumza na Mtanzania Digital.

Amesema wasichana hao ni wale waliomaliza elimu ya msingi na kushindwa kuendelea na masomo.

Nestory amesema kuwa wasichana walionufaika na mpango huo ni wale wanaoishi katika mazingira magumu, ambao hawawezi kuendelezwa kielimu na familia zao.

Mkurugenzi huyo ametaja mafunzo waliyopatiwa kuwa ni ya Ushonaji, Mapambo, Mapishi pamoja na Ufundi selemala.

wasichana hao wamepelekwa katika vyuo tofauti tofauti kulingana na kozi wanazochukua ikiwemo Chuo cha Ufundi Stadi – VETA Kagera, VTC Karagwe, VTC Kagondo, Nyakato mkoani Mwanza na Sengerema.

Amesema baada ya kupata fani hizo Shirika la Humuliza linatoa vitendea kazi kwao ikiwamo vyerehani, vyombo vya mapishi, vifaa vya mapambo pamoja na vifaa vya uselemala ili kuwawezesha kuendeleza kwa vitendo fani walizopata.

“Shirika la Humuliza limekuwa likijihusisha na watoto kuanzia mwaka sifuri mpaka miaka 17 kuwasaidia katika nyanja mbalimbali ikiwemo na msaada wa kisaikolojia.

“Tunatoa pia misaada ya kijamii na kisaiklojia kwa watoto wanaoishi katika mazingira duni wanaokuwa wamefiwa au kutelekezwa, na wanaoishi katika familia zenye migogoro, kwa kushirikiana na jamii inayowazunguka, lengo wapate mahitaji yao,” amesem Nestory.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles