25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Bilionea Jeff Bezos ajiuzulu kuwa mkurugenzi wa Amazon

New York, Marekani

Mwanzilishi wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos(57), amejiuzulu katika wadhifa wake wa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya biashara ya mtandaoni ambayo ilianza katika gereji yake karibu miaka 30 iliyopita.

Bezos sasa hivi atakuwa mwenyekiti, hatua aliyosema itampa “muda na nguvu zaidi” kuangazia biashara zake zingine.

Nafasi ya Bezos, ambaye ni miongoni mwa wanaume tajiri zaidi duniani, itachukuliwa na Andy Jassy, ambaye sasa hivi anaongoza biashara ya uhifadhi wa data.

Andy Jassy

Mabadiliko hayo yatafanyika katika kipindi cha nusu ya pili cha mwaka 2021, taarifa kutoka kampuni hiyo imesema.

“Kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Amazon ni majukumu muhimu na yenye kuhitaji muda. Ukiwa na jukumu kama hilo. Ni vigumu sana kutoa angalizo kwa mambo mengine,” Bezos amesema katika barua aliyoituma kwa wafanyakazi wa kampuni ya Amazon siku ya Jumanne.

“Kama mwenyekiti nitakuwa najihusisha na mambo mengine muhimu ya kampuni ya Amazon lakini pia nitakuwa na muda na nguvu ya kuangazia miradi ya Day 1 Fund, Bezos Earth Fund, Blue Origin, The Washington Post, na mingine ninayotaka kuikuza zaidi.

“Sikuwa na nguvu inayohitajika lakini hilo halina uhusiano wowote na kustaafu. Nina shauku kubwa juu ya kile ambacho nafikiria kuwa kinaweza kutimizwa na kampuni hii,” aliongeza.

Bezos, ameongeza kuwa kampuni ya Amazon tangu ilipoanza biashara ya uuzaji wa vitabu mtandaoni 1994.

Kampuni hiyo yenye wafanyakazi milioni 1.3 kote duniani na yenye kujihusisha na karibu kila kitu kuanzia kufungasha kwa bidhaa, huduma za video, uhifadhi wa data na biashara.

Bezos anadaiwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 196.2, kwa mujibu wa orodha ya mabilionea wa jarida la Forbes.

Kampuni hiyo iliendelea kuimarika zaidi mwaka jana wakati janga la corona lililopokuwa linaendelea kusambaa na kusababisha kuongezeka kwa manunuzi ya mtandaoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles