24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Bilione Laizer awa kivutio kwa wananchi Dar

 CHRISTINA GAULUHANGA -DAR ES SALAAM 

BILIONEA wa Madini ambaye ni mchimbaji mdogo wa Madini Merelani mkoani Manyara, Saninilu Laizer jana alikuwa kivutio katika Maonyesho ya Biashara ya 44 ya Kitaifa Sabasaba baada ya kufikia katika viwanja hivyo na kumtembelea mabanda mbalimbali huku akinunua bidhaa kadhaa. 

Bilionea huyo alifika katika viwanja hivyo saa 4 asubuhi akiwa kwenye gari aina ya Land Cruiser akiwa ameambatana na watendaji wa Tume ya Madini , Viwanda na Biashara, Chama cha Msalaba Mwekundu, skauti pamoja na wananchi mbalimbali waliohudhuria katika Maonyesho hayo. 

Akizungumza mara baada ya kufanyia ziara fupi ya kumtembelea mabanda mbalimbali katika Banda la Tume ya Madini, Katibu Mtendaji wa Tume ya hiyo, Profesa Shukrani Manya alisema, upatikanaji wa madini ya Laizer ni matokeo ya ujenzi wa ukuta wa Mirerani na uwepo wa miundombinu wezeshi ya vituo vya madini katika mikoa mbalimbali. 

Alisema awali wachimbaji wadogo walikuwa wakidhurumiwa madini yao kwa sababu ya kukosekana ulinzi na masoko ya uhakika lakini kwa sasa Serikali imejiimarisha na kila mchimbaji ananufaika na anachokipata. 

“Serikali inafanyakazi kwa sababu ya ilani ya chama chao ndio kila kitu kinachoelekezwa ni lazima kifanikiwa hivyo hata upatikanaji wa madini na utunzaji mazingira sehemu za migodi ni moja ya maelekezo ya chama hicho,” alisema Prof. Manya. 

Alisema anashukuru upatikanaji wa madini yenye uzito wa gramu 14.13 ya Laizer yenye thamani ya Sh bilioni 7.7 yamekuja muda muafaka kukiwa na ulinzi na ndio maana ameweza kunufaika nayo. 

Alisema awali wachimbaji wengi walikuwa wakikutana na matapeli na kuwadhurumu madini yao wachimbaji. 

Manya alisema katika miaka michache ya uwapo wa tume wamefanikiwa kuwarasimisha wachimbaji wadogo na kuwagawia maeneo hayo ambayo yamesaidia kuleta matokeo mazuri tofauti na miaka ya nyuma ambapo mengi yalikuwa yakifanyika tafiti na kuacha. 

Kwa upande wake, Laizer aliishukuru serikali kwa kujenga ukuta huo kwa sababu umesaidia kupata thamani halisi ya madini yake aliyoyapata. 

“Isingekuwepo ukuta ningeweza kukutana na mtu akanidanganya na kunipa fedha ndgo kisha kutokomeza,” alisema Laizer. 

Alisema kwa sasa kimekuwa na uhuru wa kutosha wamekuwa wakifanya shughuli zao kwa amani ambapo asilimia 10 ya Mapato wanayoyapata wanawaoa wafanyakazi wao. “Nawaomba Watanzania wenzangu waje huku kuchimba madini kwani kuna uhakika wa fedha na kuna fursa kwakuwa hata yeye ametoka kwenye familia maskini lakini kwa sasa amejikwamua,” nalisema Laizer. 

Laizer aliiibuka bilionea Juni mwaka huu baada ya Rais kumtambua rasmi na kununua madini yake ya Tanzanite yenye thamani ya Sh bilioni 7.7 ambayo madini hayo hayajawahi kupatikana tangu uchimbaji wa Mirerani uanze na kuweka historia ya mawe hayo mawili kununuliwa. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles