28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

BIL. 4/- KUBORESHA LISHE YA WANAWAKE, WATOTO

Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nutrition International,  Joel Spicer

Na ARODIA PETER-DAR ES SALAAM

TAASISI ya Kimataifa ya Lishe (Nutrition International), iliyokuwa ikijulikana kama Micronutrient Initiative imezindua program mpya ya ‘Right Start Initiative’ Tanzania kwa lengo la kuboresha lishe na afya kwa wanawake, wasichana wadogo pamoja na watoto wachanga.

Program hiyo ya miaka mitano imetengewa Dola za Marekani millioni 2.8 (sawa na Sh bilioni 4.7).

Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Nutrition International,  Joel Spicer alisema Dar es Salaam jana kuwa, programu hiyo imelenga kupunguza tatizo la upungufu wa damu kwa makundi yaliyotajwa hapo juu pamoja na kutatua tatizo la kudumaa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

“Pia watoto wachanga 90,000 watakuwa na mfuko utakaowasaidia wakati wa kuzaliwa, wasichana wadogo 94,000 kuongezewa vidonge vya madini ya chuma na Folik Acid kila wiki na kupewa elimu juu ya lishe bora ambapo pia  watoto 366,000 chini ya miaka miwili watapewa huduma ya lishe,” alisema Spicer

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu alishukuru msaada huo ambapo alisema mpango huo ni muhimu katika kuchangia ajenda ya sasa katika maendeleo ya taifa.

Kwa hivyo napenda kutoa shukurani kwa Nutritional International na Serikali ya Canada kwa kutuletea “Right Start” Tanzania na kubahatika kuwa katika nchi chache zilizochaguliwa barani Afrika.

“Program hiyo  itatoa mchango mkubwa katika jitihada za nchi yetu kupambana na utapiamlo, lakini pia kujenga wafanyaka zi wenye nguvu ili kusaidia ajenda yetu ya taifa la viwanda,” alisema Ummy

Hii itakuwa programu kubwa zaidi itakayofanywa na shirika la Nutrition International nchini Tanzania tangu shirika lilipofungua ofisi zake Dar es Salaam Septemba 2016.

Mradi huo niwa miaka mitano utatekelezwa katika mikoa ya Mwanza na Simiyu kwa kuwafikia wajawazito 130,000 ambao wataongezewa vidonge vya madini ya chuma na Folik Acid vilivyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles