Big Sean athibitisha kuwa Mnigeria

0
1463
Big Sean

NEW YORK, MAREKANI

RAPA anayefanya vizuri kwenye muziki huo nchini Marekani, Sean Anderson maarufu kwa jina la Big Sean, ameweka wazi kuwa ana asili ya nchini Nigeria.

Kauli hiyo aliitoa wakati anafanya mahojiano na Vibe nchini Marekani na kuthibitisha kuwa ana asili ya Afrika katika nchi ya Nigeria.

Msanii huyo ambaye amekulia katika mji wa Detroit, Michigan, amedai bibi yake mzaa mama alitokea nchini Nigeria.

“Mimi ni Mmarekani mweusi, lakini ukweli ni kwamba nina asili ya nchini Nigeria kwa kuwa bibi yangu ametokea huko na ninajivunia kuwa sehemu ya nchi hiyo,” alisema Big Sean.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here