31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

BIG SAM ACHUKUA MIKOBA YA ALAN PARDEW CRYSTAL PALACE

skysports-sam-allardyce-crystal-palace_3858160

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya England, Sam Allardyce ‘Big Sam’, ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Crystal Palace huku akichukua nafasi ya Alan Pardew ambaye amefungashiwa virago vyake.

Big Sam mwenye umri wa miaka 62, alikuwa nje ya uwanja tangu alipofukuzwa kazi na timu ya taifa ya England, Septemba mwaka huu na sasa amefanikiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili na nusu wa kuitumikia klabu hiyo ya Selhurst Park.

Kocha huyo alifukuzwa kazi ndani ya timu ya taifa ya England kutokana na tuhuma za kujihusisha na uhamisho wa wachezaji wa Ligi Kuu England na kujipatia kipato.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Bolton, Blackburn, West Ham na Sunderland, ameichukua klabu hiyo ya Palace huku ikishika nafasi ya 17, ikiwa hatarini kushuka daraja na kocha huyo anatarajia kukutana na Watford Jumatatu siku ya Boxing Day.

“Tunayo furaha kubwa kutangaza kuwa klabu ya Crystal Palace imefanikiwa kumalizana na Big Sam ambaye anakuwa ni kocha mkuu wa klabu hii, tuna imani na uwezo wake pamoja na uzoefu, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuisaidia timu hii kwenye michuano hii ya Ligi Kuu nchini England,” walisema Crystal Palace.

Hata hivyo, kocha huyo amewashukuru wahusika wa klabu hiyo kwa kufikia makubaliano yao na kumpa nafasi ya kuifundisha klabu hiyo na amedai kuwa kutokana na uzoefu wake anaamini anaweza kutoa mchango mkubwa.

“Crystal Palace ni klabu kubwa katika michuano ya Ligi Kuu nchini England, ninayo furaha kubwa kupewa nafasi ya kuifundisha klabu kubwa kama hii, kikubwa ni ushirikiano ili kuweza kuifanya klabu hii ifikie malengo yake.

“Nina uzoefu mkubwa wa Ligi Kuu nchini England, hivyo natarajia kupambana kuleta furaha kwa mashabiki wa klabu hii pamoja na kutimiza malengo niliyojipangia.

“Nina imani na wachezaji waliopo, lakini wakati wa Januari mwakani kuna uwezekano wa kuongeza wachezaji wengine ili kukiongezea nguvu kikosi hiki,” alisema Big Sam.

Kocha huyo amedai kuwa alikuwa nje ya uwanja tangu Septemba lakini alikuwa anafuatilia soka jinsi linavyokwenda, hivyo hana wasiwasi kupewa nafasi katika klabu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles