29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Bifu la Seluk, Guardiola linavyomtesa Toure

guardiola-yaya-agent-main

DOREEN PANGANI NA MITANDAO

HUENDA wakala wa  kiungo wa timu ya Manchester City, Yaya Toure, Dimitri Seluk,  alikuwa sahihi  kuhusu jambo moja tu, kwamba kocha wa timu ya  Manchester City, Pep Guardiola, ni mfalme wa klabu hiyo kwa sasa.

Wakala huyo anaona namna anavyofanyiwa mteja wake kuwa ni dhambi na  kuanza  kupambana kwa maneno, badala ya kufanya maridhiano na kocha huyo.

Seluk ni bora angekubali udhaifu na kuomba msamaha kuliko kushindana na kocha huyo, ambaye ana mamlaka kwa mteja wake (Toure).

Guardiola ndiye alikuwa wa kwanza kuanzisha uhasama kwa kujibu tuhuma za Seluk, kuhusu kukosekana kwa Toure katika michezo kadhaa, ukiwamo wa Kombe la Ligi ya England (EPL). Manchester City wamekuwa katika hali ya kutofautiana mtazamo na Seluk kwa miaka kadhaa, kwani aliwahi kufanya hivyo hata kwa kocha wa zamani wa timu hiyo, Manuel Pellegrini, ingawa  kocha huyo hakujali maneno ya shombo  ya wakala huyo. Wakala huyo alimshambulia Pellegrini kwa kumweleza kuwa alikuwa chanzo cha timu hiyo kufanya vibaya katika michezo yake ya mwisho kabla hajatimuliwa. Kutokana na mwelekeo wa Pellegrini katika timu hiyo, haikushangaza hata alipotimuliwa, hata hivyo hakuna  aliyejali kuhusu  vijembe vya Seluk kwa kocha huyo.

Kwa hali inavyoendelea sasa klabuni hapo, muathirika mkubwa ni Toure, kwani tangu msimu uanze amecheza  mchezo mmoja pekee na tayari kocha wake, Guardiola amemweleza hataweza kucheza hadi wakala wake aombe  msamaha.

Inaweza kuwa  rahisi kusema kwamba ni sahihi kwa nyota huyo kupokea kiasi cha pauni 225,000 kwa wiki, lakini anatakiwa kucheza ingawa kwa sasa ana umri wa miaka 33 na mwishoni mwa msimu atakuwa akimaliza mkataba wake wa kuchezea timu hiyo, pengine wakala wake angependa kumuona akicheza timu nyingine.

Kitu cha kushangaza zaidi ni hatua ya Seluk kuendeleza malumbano na kocha Guardiola kwa kumweleza kocha huyo anatakiwa kuiongoza Sunderland, kwani inaweza ikawa njia mojawapo ya kukubali ukweli kwamba alikosea na kuwa tayari kuomba msamaha.

Hata hivyo, Seluk anasema kuwa kama Guardiola angemchukulia Toure kama mchezaji wa kawaida, basi angeweza kutoka katika klabu hiyo kipindi alichotolewa kipa Joe Hart.

Kama Guardiola angekuwa na uhusiano mzuri na mchezaji wake huyo alipokuwa Barcelona, basi klabu hiyo ingeacha milango wazi kwa ajili ya wachezaji wengine kwa kuwa Touré alihakikishiwa kucheza lakini si kila wiki.

“Je, huku si kudhalilishana?” anahoji  Seluk na kuongeza kuwa inategemea na itakavyochukuliwa hali hiyo.

Licha ya Pellegrini kutokuzungumza chochote kuhusu nyota huyo, kulikuwa na dalili zilizoonesha Toure hakuwa na uwezo kama zamani, kwani ukiangalia umri wake na maendeleo yake uwanjani  inampasa awe mkweli, kwani ndicho Manchester  City wanachotaka.

Pengo la Toure uwanjani limekuwa halionekani baada ya Guardiola kumnunua Ilkay Gundogan.

Wachezaji wa klabu hiyo, wamekuwa wakiendelea na kazi zao za kimichezo na si kuwaza Toure atarudi lini, bali kujiuliza kama Leroy Sané na Gabriel Jesus watarudi kwenye klabu.

Hata kama Seluk na wachezaji wake wakiomba msamaha kwa Guardiola katika uwanja wa Manchester, bado Toure atapata michezo michache katika msimu huu. Japokuwa Guardiola ameshaonesha msimamo wake, bado Seluk halioni hilo, kwani mara kadhaa amekuwa akifanya kosa hili.

Wakati Guardiola akihangaika na Manchester City katika msimu wake mpya, Mourinho anaonekana akitafuta  njia nyingine ya kuipatia Manchester  United ushindi.

Kabla ya Guardiola kugombana na wakala wa Touré, alikuwa ameshawafunga United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles