BIEBER, HAILEY WAKANUSHA KUFUNGA NDOA

0
1288

NEW YORK, MAREKANI

MWISHONI mwa wiki iliyopita kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa na taarifa kwamba staa wa muziki wa pop nchini humo, Justin Bieber na mpenzi wake, Hailey Baldwin, wamefunga ndoa kimya kimya, lakini mrembo huyo amekanusha.

Mrembo huyo tayari amevishwa pete ya uchumba na wawili hao wakatangaza kuwa wanatarajia kufunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu, lakini kukaenea taarifa za kufunga ndoa kimya kimya.

Hailey alitumia ukurasa wake wa Twitter na kukanusha taarifa hiyo huku akisema kuwa endapo watakuwa tayari kufunga ndoa hakutakuwa na siri yoyote.

“Ninajua wapi taarifa hizo zilikotoka, lakini ukweli ni kwamba taarifa hizo hazina ukweli, kama tutaamua kufunga ndoa basi lazima tuweke wazi, hakuna sababu ya kufanya mambo kwa siri, hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi,” aliandika mrembo huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here