26.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Bieber akanusha kutoka na Kourtney

justin-bieber-kourtney-kardashian-nuova-coppia-di-bffNEW YORK MAREKANI

MSANII wa muziki wa Pop nchini Marekani, Justin Bieber, ameweka wazi kwamba hana uhusiano wa kimapenzi na dada wa Kim Kardashian, Kourtney ila ni marafiki wa kawaida.

Mwishoni mwa mwaka jana wawili hao walikuwa wanaonekana viwanja mbalimbali vya starehe na kuacha maswali mengi kwa watu mbalimbali ambapo kwenye mitandao ya kijamii kulivuma kwamba wanatoka kimapenzi.

Hata hivyo, Bieber amekanusha na kudai kwamba hakuna uhusiano wowote kimapenzi zaidi ni urafiki wa kawaida.

“Ukaribu wa mimi na Kourtney umekuwa na maswali mengi, wengi wanadhani kwamba ninatoka na mrembo huyo, lakini ukweli ni kwamba ni rafiki wa kawaida na ananiagiza kumfanyia baadhi ya mambo yake,” alisema Bieber.

Bieber ana umri wa miaka 21, wakati huo Kourtney ana umri wa miaka 36, hivyo iliwapa watu maswali mengi kwamba kwanini mrembo huyo anawapenda vijana wenye umri mdogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles