NEW YORK, MAREKANI
MKALI wa muziki wa pop nchini Marekani, Justin Bieber, ameifuta akaunti yake ya mtandao wa Instagram baada ya mpenzi wake kutukanwa na mashabiki.
Msanii huyo raia wa Canada na mpenzi wake wa zamani, Selena Gomez, walikuwa wakishtumiana kwenye mtandao baada ya nyota huyo kumtambulisha mpenzi wake mpya, mtoto wa Lionel Richie, Sofia Richie.
Kutokana na kitendo cha wawili hao kurushiana maneno, baadhi ya mashabiki walitumia akaunti hiyo ya Instagram kuandika maneno ya kuudhi, jambo ambalo lilimkera msanii huyo akatangaza kuifunga akaunti yake hiyo ili akwepe matusi hayo.
Hata hivyo, Selena alisema kama hataki kutukanwa asiweke picha za watu wake anaowapenda kwenye akaunti yake,” aliandika Selena.