30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Bieber afunguka alivyoacha dawa za kulevya

Los Angeles, Marekani

MSANII wa muziki wa Pop nchini Marekani, Justin Bieber, ameanika jinsi alivyoacha kutumia dawa za kulevya pamoja na uvutaji wa bangi.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 25, amesema alianza kuvuta bangi huku akiwa na umri wa miaka 13, ikiwa jina lake linakuwa kwa kasi.

“Nilipata jina nikiwa na umri mdogo, hivyo nikaanza kuvuta bangi, kunywa pombe na kutumia dawa za kulevya, baadae nikajua kuwa ninaelekea kubaya, wazazi wangu hawakunijengia misingi imara, hivyo ningeweza kupoteza maisha.

“Watu wengi hawakujua jinsi gani nipo kwenye wakati mgumu, lakini baada ya kujitambua, ila siku moja niliamka na kumuomba Mungu aniongoze, huku nikisema kama kweli ataniongoza basi nitaamua kuachana na vitu hivyo hadi mwisho wa maisha yangu, nashukuru nimefanikiwa,” alisema msanii huyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles