23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

….Biden ndiye mtu anayeweza kumuondoa madarakani

 WASHINGTON, Marekani

JOE Biden ndiye mtu pekee anayeweza kumuondoa madarakani Rais Donald Trump wa Marekani ambaye anawania miaka minne zaidi katika Ikulu ya White House.

Kwa wafuasi wake, yeye ni mtaalamu wa sera za kigeni na mzoefu wa miongo kadhaa Marekani, katika kuhutubia umma kwa haiba rahisi inayeweza kufikia watu wa kawaida.

Biden ni mtu ambaye jasiri aliyepitia majanga makubwa katika maisha yake.

Kwa wakosoaji wake, yeye ni mtu aliye juu-ya-kilima anayepambana kupata ushawishi.

Biden si mgeni katika kampeni – alianza kuwa seneta mnamo 1973 (miaka 47 iliyopita) na kampeni yake ya kwanza ya urais ilianza mnamo 1987 (miaka 33 iliyopita).

Ni mtu anayependa kuzungumza sana mbele ya umati, anazungumza haraka sana..anaweza kumaliza kampeni kabla ya muda wa kumaliza.

Biden anapenda kuzungumza katika umma ingawa huwa anatengeneza vichwa vya habari visivyoeleweka wakati mwingine

Kwenye mikutano ya hadhara alianza kudai: “Wazee wangu walifanya kazi katika migodi ya makaa ya mawe kaskazini mashariki mwa Pennsylvania” na kwamba alikuwa na hasira hawakupata fursa katika maisha waliyostahili.

 Lakini hakuna hata mmoja wa ndugu zake ambaye alikuwa mchimbaji wa makaa ya mawe – alikuwa ameiba maneno hayo kutoka kwa hotuba ya mwanasiasa wa Uingereza Neil Kinnock ambaye jamaa zake walikuwa wachimbaji.

Akijisifu juu ya uzoefu wake wa kisiasa, mwaka huu 2012 aliwaambia umati: “Jamani, naweza kuwaambia nimewajua marais wanane, watatu kati yao nimekuwa na uhusiano nao wa ukaribu,” kwa bahati mbaya akimaanisha alikuwa akifanya mapenzi nao badala ya kuwa marafiki wa karibu tu.

Akiwa Makamu wa Rais wa Barack Obama, mwaka 2009 aliwapa watu hofu kwa kudai kuwa kulikuwa na “asilimia thelathini ya kushindwa katika uchumi”.

Na labda alikuwa na bahati ya kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza wa rais mweusi wa kwanza baada ya kumuelezea Barack kuwa wa ajabu “Mwafrika wa kwanza wa Marekani mwerevu, msafi na muonekano mzuri”.

Licha ya maoni hayo, msaada wa Biden kati ya wapiga kura weusi umekuwa mkubwa sana wakati wa kampeni ya urais ya sasa, lakini hivi majuzi kumekuwa na gumzo kwenye kipindi kilichoendeshwa na mtangazaji wa redio mwenye asili ya Afrika, Charlamagne Tha God kiliibua taharuki baada ya kudai: “Ikiwa unapata shida kujua utampigia nani kura kati yangu na Trump, basi wewe sio mweusi. “

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles