33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Biden atofautiana na Trump, Kenosha

 MGOMBEA urais kupitia chama cha Democratic Joe Biden amewaambia wakazi wa Kenosha katika jimbo la Wisconsin kwamba hali tete iliyojitokeza katika siku za karibuni kwenye eneo hilo inaweza kuwasaidia Wamarekani kubadili uongozi kupinga ubaguzi wa rangi.

Machafuko yameukumba mji wa Kenosha kufuatia tukio la polisi kumpiga risasi Mmarekani mweusi Jacob Blake.

Biden amesema hali hiyo inaweza kuwasaidia wamarekani kukabiliana na ubaguzi wa kimfumo uliodumu miongo kadhaa nchini humo, matamshi ambayo yanatoafutiana kabisa na Rais Donald Trump.

Biden amesema kwenye kanisa la Kilutheri la Grace ambako alikutana na viongozi wa eneo hilo baada ya kikao cha faragha na Blake pamoja familia yake kwamba hatimaye Wamarekani sasa wamefikia mahali ambapo watatakiwa kushughulikia alichokiita ‘’dhambi ya asili’’ ya taifa hilo, utumwa pamoja na mabaki yake yote.

Ziara hiyo iliashiria safari ya kwanza ya makamu huyo wa rais wa zamani kwenye eneo linalokabiliwa na machafuko katika jimbo la Wisconsin, kama mgombea mteule wa urais kupitia chama cha Democratic na ilikuwa kielelezo cha wazi kabisa kinachoonyesha tofauti kati yake na Trump.

Wakati Biden akiwa ametumia zaidi ya saa moja akiwa na familia ya Blake, Trump hakuthubutu hata kumtaja Blake alipokuwa ziarani mjini Kenosha siku ya Jumanne.

 Huku Biden akisema matatizo yanayoshuhudiwa katika mfumo wa sheria yalianza enzi ya utumwa nchini Marekani, Trump alikataa kukiri kuhusu ubaguzi wa kimfumo na badala yake akaonyesha kuunga mkono waziwazi vyombo vya sheria, huku akiyataja machafuko hayo kuwa ni ugaidi wa ndani.

Rais Donald Trump anayafananisha machafuko ya Kenosha na ugaidi wa ndani, na kutofautiana na Biden.

Biden amemkosoa Trump kutokana na madai yake dhidi ya waandamanaji, kujitetea kwamba anatumia sheria na kukanusha kwamba Wamarekani wenye ngozi za nyeusi wanakabiliwa na vizingiti, tofauti na weupe. Akasema, matamshi ya rais yanaweza kuharibu ama kuleta amani.

Alisema “Kama ninaweza kutoa hoja ya kawaida, matamshi ya rais yana uzito, haijalishi ni mazuri, mabaya au ya kujali, ni muhimu. Haijalishi rais ana uwezo gani au hana uwezo, anaweza kupeleka taifa vitani. Anaweza kuleta amani.

Anaweza kufanya masoko kupanda au kushuka. Na anaweza kufanya vitu ambavyo nimeona vinaweza kuleta mabadiliko kwa kile anachosema tu.”

Blake bado yuko hospitali baada ya kupigwa risasi mgongoni mara saba na polisi mzungu katika mji wa Kenosha, wakati walipokuwa wakijaribu kumkamata Agosti 23 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles