25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Biden ashinda jimbo la South Carolina

WASHINGTON, MAREKANI

Joe Biden amepata ushindi mkubwa katika kura ya uteuzi wa mgombea wa chama cha Democratic jimboni South Carolina akipata kuungwa mkono na Wamarekani weusi na kufikisha mwisho ushindi mfululizo wa Bernie Sanders.

Ushindi wa  Biden umekuja katika wakati wa kufa na  kupona  katika mwaka  2020 wakati  mwanachama  huyo wa chama cha Democratic  mfuasi  wa  siasa  za  wastani akirejea  katika  mbio hizo  baada  ya kushindwa katika  majimbo  ya  Iowa, New Hampshire  na  Nevada.

Mbio hivi  sasa zinaingia  katika  awamu mpya  wakati  majimbo 14 yatakapoanza rasmi  kampeni  katika  kile kinachofahamika  kama  Jumanne Kuu.

“Bado tuko  hai. Kwa nyie wote ambao  mmeanguka, jihesabuni mmeondolewa, mmeachwa nyuma , hii  ndio  kampeni  yako,” Biden  alisema  katika  mkutano  wa  baada  ya uchaguzi.

Sanders  amepata nafasi  ya  pili, licha  ya  kuwa  kushindwa  kwake kumetoa  ahueni  ya  muda kwa  wademokrat wenye shauku ambao wanahofia  kuwa mwanasiasa  huyo  aliyejitangaza  kuwa ni msoshalist ataibuka mwezi Februari  kwa  ushindi  wa  majimbo manne.

Mwanaharakati  tajiri, bilionea Tom Steyer , ambaye  alikuwa akipambana  ili  kupata  nafasi  ya  tatu, amesitisha  rasmi  kampeni yake.

Alitumia  zaidi  ya  dola milioni 19 katika  matangazo  ya televisheni   katika  jimbo  la  South Carolina, fedha  nyingi  zaidi kuliko wapinzani wake  wote  kwa  jumla, lakini  hakuweza  kupata njia katika  mpambano  huo wenye  wagombea  wengi.

Wagombea saba  wanaendelea  na  mbio zao kutaka  kuteuliwa  na chama  cha  Democratic  kupambana  na  rais wa  sasa  Donald Trump mwezi Novemba.

Washirika  wa  Biden haraka  waliuelezea  ushindi  huo  wa  South Carolina  kuwa  ushahidi  kuwa  anapaswa  kuwa  mgombea  wa chama  hicho  akiwa  ni  mbadala  wa  wazi  wa  Sanders.

Uchaguzi  wa  mchujo  katika  jimbo  la  South Carolina  ni mtihani wa kwanza  mkubwa kwa  wagombea  miongoni  mwa  wapiga  kura weusi.

Na  kwa  kuwa  umempa  Biden  mwenye  umri  wa  miaka  77 ushindi  ambao  alikuwa  akiuhitaji  mno, ni  lazima  athibitishe  kuwa ana vitendea  kazi pamoja  na  uwezo wa  kifedha  kupanua  kampeni yake  katika  muda  wa  masaa  72 yajayo.

Pia atakuwa  katika shinikizo kutegemea  uhusiano wake  wa  muongo  mmoja  na viongozi wa  chama kutengeneza hali  mpya ya kwamba inawezekana  katika  kugombea  kwake.

Shirika la  habari  la  Associated Press lilitangaza  Joe Biden mshindi , muda  mfupi tu  baada  ya  upigaji  kura  katika  jimbo  la South Carolina.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles