30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Bia ya Safari kinara kwa ubora Afrika

safari

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya TBL Group imezidi kung’ara  kutokana na viwanda vyake vya kutengeneza bia   Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Arusha  kushinda tuzo za juu za mataifa za SABMiller Afrika.

Viwanda hivyo vimeibuka kidedea kwa uzalishaji bora ambako pia bia   ya Safari imetangazwa kuwa   bora barani Afrika  (Champion Beer).

Mkurugenzi wa Ufundi wa TBL Group, Gavin Van Wijk amevipongeza viwanda vyote kwa kuibuka na ushindi wa tuzo kubwa za SABMiller.

“Ushindani ulikuwa mkubwa ukihusisha viwanda vingine kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

“Inafurahisha kuona viwanda vya Tanzania vinachomoza na kushinda tuzo kama hizi.

“Hii inadhihirisha kuwa TBL imejipanga kwenda sambamba na mkakati wa serikali wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa kuwa mafanikio haya yanaletwa na Watanzania wenyewe,” alisema Wijk.

Kampuni ya SABMiller imekuwa na utaratibu wa kushindanisha viwanda vyake katika nchi mbalimbali na kutoa vigezo vya kushindania huku kigezo kikubwa kimoja kikiwa ni ubora wa bidhaa zinazozalishwa.

Hafla ya kutangaza viwanda vilivvoshinda na kuvipatia tuzo ijulikanao kama ‘SABMiller Africa Technical Awards’ ilifanyika  Afrika Kusini juzi   na kuhudhuriwa na maofisa waandamizi na mameneja wa viwanda vya bia kutoka kampuni zake tanzu.

Safari Lager inayozalishwa katika viwanda vya TBL vya Dar es Salaam na Arusha ilitangazwa kuwa ni bia bora barani Afrika na kutunukiwa tuzo huku kiwanda  cha Dar es Salaam kikiwa kimeshika nafasi ya kwanza na Arusha nafasi ya pili.

 

Tuzo nyingine ambazo viwanda vya TBL Group vimeshinda ni tuzo ya uzalishaji wa bia bora ya Castle inayojulikana kama Mick Steward Castle Lager award ambako kiwanda cha TBL Dar es Salaam pia kilishika nafasi ya kwanza,TBL Mbeya nafasi ya pili na TBL Arusha nafasi ya tatu.

 

Nyingine ni Tuzo ya Upishi Bora wa bia ya mwaka (Brewery of the Year Award), ambaKo kiwanda cha TBL Mbeya

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles