Beyonce urembo namba mbili duniani

0
1157

NEW YORK, MAREKANI

DAKTARI bingwa wa upasuaji nchini Uingereza, Julian De Silva, ameianika orodha ya wasichana warembo duniani huku mke wa rapa Jay Z, Beyonce akishika nafasi ya pili kwa uzuri huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Bella Hadid.

Bella mwaka 2016 alitwaa tuzo ya mrembo bora wa mwaka, hivyo De Silva ameweka wazi kwamba, hakuna upasuaji wa urembo wa kisasa ambao utafanyika na kuzizidi sura za warembo hao wawili.

“Urembo wa msichana unapimwa kwa muonekano wake, hata hivyo hawezi kupita asilimia 94.35, Beyonce yeye anakaribia asilimia 92.44, akizidiwa na Bella Hadid.

“Kwa vipimo vya urembo Beyonce ni wazi anashika nafasi ya pili duniani akizidi wan a Bella na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Amber Heard mwenye umri wa miaka 33, ambaye ana asilimia 91.85, wakati huo Ariana Grande na Taylor Swift wakishika nafasi ya nne na tano,” alisema mwanasayansi huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here