BEYONCE: MAVAZI HAYANIPENDEZI KWA SASA

0
880

LOS ANGELES, MAREKANI


NYOTA wa muziki nchini Marekani, mke wa rapa Jay Z, Beyonce, amefunguka kwamba ujauzito wake unamfanya asipendeze na mavazi anayoyavaa.

Mrembo huyo, ambaye anatarajia watoto wawili mapacha, juzi alitoka na mume wake, Jay Z na kuhudhuria sherehe za Wearable Art Gala, mjini Los Angeles, ambapo mashabiki wake wengi walionekana wakimshangaa.

Beyonce anaamini mashabiki hao walikuwa wanamshangaa mwonekano wake wa mavazi ulivyo kwa sasa, hasa kutokana na ujauzito.

“Mashabiki wengi wanajua kuwa nina ujauzito, ila ninaamini kunishangaa kwao si kwa kuwa nina ujauzito, ila ni kutokana na mwonekano wa nguo zangu kwa sasa, nadhani haupendezi na ndiyo maana wananitolea macho sana,” alisema Beyonce.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here