24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

BEYONCE, JAY-Z WAONYESHA JEURI YA FEDHA

ROME, ITALIA


MASTAA wa muziki nchini Marekani, Jay Z na mke wake Beyonce, wameonyesha jeuri ya fedha kwa kukodi boti la kisasa kwa dola milioni 1.4 kwa wiki ikiwa ni zaidi ya Sh bilioni tatu za Kitanzania.

Wanandoa hao ambao kwa mujibu wa mtandao wa Forbes, mwaka jana waliweza kuingiza kiasi cha dola milioni 147 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 332 za Kitanzania kutokana na kazi zao za muziki.

Kwa sasa wawili hao wapo nchini Italia kwa ajili ya mapumziko ya ziara yao ya muziki ijulikanayo kwa jina la ‘On The Run II’, hivyo wameonekana wakiwa na boti hilo.

Sifa ya boti hilo ni pamoja na kuwa na sehemu ya swimming pool, uwanja wa kuchezea kikapu, Gym, vyumba vya kulala, ukumbi wa sinema, sehemu ya familia kula chakula, saloon na chumba cha kufanyia mazoezi ya muziki.

Boti hilo linatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 180, zaidi ya Sh bilioni 407 za Kitanzania, inamilikiwa na tajiri kutoka nchini Marekani, Shahid Khan ambaye anamiliki timu ya NFL, Jacksonville Jaguars.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,859FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles