25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

BEYONCE AANGUKA JUKWAANI

CALIFONIA, MAREKANI


MWANAMUZIKI wa Marekani, Beyonce Knowles, mwishoni mwa wiki iliyopita alishindwa kumaliza onesho lake akiwa jukwaani baada ya kuteleza mguu wa kushoto na kuanguka pamoja na  mdogo wake, Solange, katika  tamasha la muziki la Coachella linalofanyika jijini Califonia, Marekani.

Beyonce baada ya kufanya vizuri katika onesho la  wiki iliyopita, juzi aliungana na Solange, jukwaani kuimba wimbo wa  ‘Get Me Bodied’, lakini walishindwa kumalizia baada ya kuteleza na  kuanguka wakati akijaribu kumbeba.

Mwanamuziki huyo wiki iliyopita aliungana na kundi lake la zamani  la Destiny’s Child, linaloundwa na  Michelle Williams na Kelly Rowland.

Mara ya mwisho, Destny’s Child kuimba pamoja ilikuwa mwaka 2013, baada ya kutengana mwaka 2003.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles