23.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Betika yazindua SODO 4 C LIMATE

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya michezo ya kubashiri Tanzania Betika kampeni ya Sodo 4 Climate, katika kampeni hii betika wanahamasisha utunzaji wa mazingira kupitia mchezo wa sodo.

Kauli mbiu ya kampeni hiyo wakiwa wameipa jina la “Shabikia soka sio uharibifu wa mazingira”.

Akizungumza na waandishi wa habari Februari 22, jijini Dar es Salaam Meneja Mkuu wa Betika, Tumaini Maligana katika uzinduzi huo amesema kuwa.

“Lengo ni kupambana kupunguza mabadiliko ya tabia za nchi kwa ujumla, kupitia utunzaji wa mazingira basi tutahakikisha hali ya hewa nzuri, afya bora na pia maendeleo katika jamii yetu,” amesema Maligana.

Katika sodo 4 climate itachezeka ligi katika soka la ufukweni wa Coco Beach ambapo Betika wamealika jumla ya timu 8 zitakazoshiriki na ligi hii itaenda kwa muda wa takribani wiki saba. Ligi hii itahusisha team zifuatazo, Betika staff fc, Coco beach FC, RC FC, Tulia trust foundation FC, Espanyol fc, Bodaboda msasani FC, Ipp media. Katika ligi hii pia kila team watakua na team za wanawake na wanaume ambazo kila jumamosi kutakua na mechi moja ya wanawake na mechi moja ya wanaume.

“Ufunguzi wa ligi hio ulitanguliwa na usafishaji wa mazingira kwa ujumla na pia kutoa elimu kuhusiana na swala zima la kuhifadhi taka katika maeneo husika. Katika kipindi cha wiki zote saba za ligi hiyo kutakua na matukio mbali mbali ya utunzaji wa mazingira na maendeleo ya kijamii kwa ujumla,” amesema.

Meneja Tumaini alimalizia kwa kuwatakia kila la kheri timu zote zitakazo shiriki katika ligi hii ya Sodo 4 Climate kwa sababu betika watatoa zawadi za kutosha kwa wale watakaofika fainali ya Sodo 4 Climate, mechi ya ufunguzi ilikua Betika staff fc 1- 3 Coco Beach FC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,184FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles