Betika yazindua kampeni mpya kuelekea AFCON

Na Mwandishi Wetu 

KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya Betika kwa ushirikiano na kampuni ya simu Tigo, imezindua kampeni  inayoitwa ya ‘Twenzetu Ivory- Coast Ki-VIP’

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 6,2023 Jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa kampuni hiyo, Juvenalius Rugambwa amesema kampeni hiyo ni kwa ajili ya wateja wao wanaotumia mtandao wa tigo pekee.

“Betika inaendelea kujali na kuwapa huduma bora wateja wake kwa kuzindua promosheni nzuri na zenye zawadi za kutosha kwa watanzania.

“Kuanzia msimu huu wa sikukuu hadi michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) itakayo anza  tarehe 4 jijini Abidjan Ivory Coast. Promosheni hii itakuwa na zawadi za TV  inchi 70 kila wiki kwa washindi 2, zikiambatana na ving’amuzi  na kifurushi cha mwezi mmoja,” amesema Rugambwa.

Ameeleza  kuwa tofauti na hivyo, kutakuwa na droo ya kila siku ya kushindania fedha, huku zawadi kubwa ikiwa  ni tiketi ya VIP   kwa mabingwa  sita watakaolekea  Ivory Coast kutazama mechi za mashindano ya AFCON.

 Amesema washindi hao sita watapata tiketi za ndege za kwenda na kurudi,  watalipiwa gharama za hotel kwa siku zote ndani na  usafiri wa kifahari kuelekea uwanjani na pia tiketi ya kutazama mechi,” amesema Rugambwa.