30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Betika yatangaza washindi wa kampeni ya ‘Mtoko Kibingwa’

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

DROO ya Kampeni ya Mtoko wa Kibingwa kwa Msimu wa 5 yaibua washindi wa 4 huku kwa mara ya kwanza  kupatikatika kwa mshindi mwanamke tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo.

Kampuni ya michezo ya ubashiri ya Betika imetangaza washindi wa droo ya kwanza na ya pili kwa msimu na kupatikana washindi wanne kutoka mkoani Songea, Simiyu, Kagera pamoja na Dar es Salaam. 

Aidha, mshindi kutoka Chamazi jijini Dar es Salaam, Mariam Mohammed(24) amesema anajisikia furaha kushinda katika droo hiyo ya mtoko wa kibingwa kwa msimu wa 5 akiwa kama mwanamke.

“Nina kawaida ya kucheza mara kwa mara lakini nilipopigiwa na kupewa taarifa kuwa nimeshinda nilifurahi zaidi,” amesema Mariam.

Mariam amesema siku ya Derby hiyo atashangilia timu zote kwani yeye hayupo kwenye timu zote mbili.

Pia amewashauri wanawake kuweka ubashiri wao kwani michezo ya ubashiri hayachagui jinsia .

Mshindi kutoka Songea mkoani Ruvuma, Constantine Mbele(26) anaejihusisha na kazi ya undereva amesema ameshiriki Kampeni hiyo kwa kuweka ubashiri wake kwa Sh elfu 3,000 kwa mikeka 5 yenye mechi 3.

“Nimeshiriki sana ubashiri kwenye Kampuni ya Betika na nimeshashinda pesa Sh 300,000 ambayo nilifanya manunuzi ya mbolea, kununua mahitaji mbalimbali. 

Aidha, Mbele ameeleza shahuku yake kubwa kufika jijini Dar es Salaam ambapo hajawahi kufika huku shahuku yake kubwa Kumuona Mchezaji Clatous Chama 

“Mimi ni shabiki wa Mnyama Simba Aprili 16,2023 natarajia makubwa kwenye timu yangu italeta ushindi dhidi ya Wapinzani wetu Yanga hivyo nategemea zaidi Chama atafunga magoli,” amesema Mbele.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, msimu huu utachukua washindi 100  na utaenda kukamilisha idadi ya washindi 500 wa Kampeni ya mtoko wa Kibingwa ambapo msimu wa kwanza walishinda washindi 400.

Kushiriki ubashiri huo ni rahisi kwa kutembelea website www.betika.com au kwa wale wenye viswaswadu kwa kubonyeza 14916#. Kwa kuweka dau la Sh 500 kwa mikeka mitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles