26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

BENZEMA: ZIDANE NI KAMA KAKA YANGU

23d954b8fb4a4e59a47742c5032fce4b

MADRID, HISPANIA

STRAIKA wa Real Madrid, Karim Benzema, amedai kuwa kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane, ni kama kaka kwake.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amecheza mechi 11 tu za La Liga msimu huu, ambapo tatu aliingia kutokea benchi.

Benzema alikabiliwa na lawama katika kampeni, lakini amefanya kazi njema katika mechi ya Real Madrid ya Kombe la Dunia la klabu ambapo walishinda dhidi ya Club America na kutinga fainali.

Mshindi wa Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo, aliisaidia timu yake kushinda kwa kufunga goli lake la 500 kwa miamba hao wa Hispania.

Baada ya mechi, Benzema aliueleza mtandao wa Teledeporte: “Zidane ni kama kaka kwangu, ni mfano kwangu na ninafurahi kufanya naye kazi.

“Haukuwa mwaka mgumu kwangu, nimecheza vizuri katika mechi mbili au tatu. Umekuwa mwaka mzuri sana, ambao nimetwaa mataji na Real Madrid na kufunga mabao mengi.”

Benzema amefunga mabao manne ya ligi msimu huu na amefunga idadi hiyo hiyo pia kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wakati klabu hiyo ikitinga fainali kucheza dhidi ya Kashima Antlers, CR7 binafsi amesherehekea goli lake la 500 tangu alipotua Real Madrid.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, tayari alikuwa ameshafikisha mabao 500 kwa klabu na nchi yake katika goli alilofunga Ureno dhidi ya Malmo hapo awali Septemba 2015 na alitimiza idadi hiyo akiwa amecheza mechi 753 tu. Lakini sasa akiwa amecheza mechi 689 Real Madrid tayari ametimiza mabao 500.

Pamoja na mabao 118 ya Manchester United katika mechi 292, mabao matano katika mechi 31 akiwa Sporting Lisbon, rekodi yake Real Madrid inasimamia mabao 377 katika mechi 367.

Takwimu hizo zinamfanya kuendelea kuwa mchezaji wa pili kufunga mabao mengi La Liga akiwa amefunga mabao 270 katika mechi 247, akiwa wa pili kwa nyota wa Barcelona Lionel Messi mwenye mabao 321 katika mechi 359.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles