32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Benzema aomba kulitumikia taifa lingine

PARIS, UFARANSA

MSHAMBULIAJI wa mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, Karim Benzema ambaye ni raia wa nchini Ufaransa, ameliomba taifa hilo kumruhusu kutafuta taifa lingine la kulitumikia katika soka.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ametuma maombi hayo baada ya kuachwa tena kwenye kikosi cha timu ya taifa Ufaransa kwenye michezo ya kufuzu kushiriki Kombe la Euro 2020.

Benzema mara ya mwisho kuitumikia timu ya taifa ilikuwa 2015, hivyo amefungiwa kuitumikia timu hiyo kutokana na kumiliki mkanda wa ngono wa mchezaji mwenzake wa timu hiyo Mathieu Valbuena, akiwa na lengo la kutaka kujipatia fedha.

Mbali na kuwa kwenye kiwango kizuri, chama cha soka nchini Ufaransa kikaachana na mchezaji huyo kuanzia kwenye michuano ya Euro 2016 kwenye ardhi ya nyumbani pamoja na Kombe la Dunia mwaka jana huku taifa hilo likichukua ubingwa.

Benzema aliomba radhi mara kadhaa lakini ombi lake hadi sasa halijasikilizwa, hivyo kutokana na hali hiyo ametumia ukurasa wake wa Twitter kuandika ujumbe ambao umemtaka rais wa shirikisho la soka nchini Ufaransa (FFF), Noel Le Graet kumruhusu atafute taifa liginge akalitumikie kisoka.

“Najua Noel hauwezi kuingilia maamuzi ya kocha, lakini nitumie nafasi hii kuweka wazi kuwa, nadhani sina tena nafasi ya kucheza soka katika taifa langu kutokana na kufungiwa, hivyo huo ndio mwisho wangu wa soka la taifa.

“Kama kweli mnaona nimemaliza hatua ya kucheza soka ndani ya taifa hilo basi niacheni nitafute nchi nyingine ambayo nitakwenda kuwa mchezaji wao alafu tuone,” aliandika mchezaji huyo kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Benzema asili yake ni kutoka nchini Algeria, hivyo hata kama ataruhusiwa na shirikisho la soka nchini Ufaransa kutafuta nchi nyingine bado atakuwa katika wakati mgumu wa kupata nchi kwa mujibu wa sheria za FIFA, kwa kuwa tayari amecheza michuano mikubwa akiwa na Ufaransa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles